Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
VURUGU kubwa zimetokea katika Shule ya Sekondari Kigonigoni wilayani
Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro, baina ya wanafunzi wa kidato cha tano na
sita na kusababisha baadhi kushikiliwa na polisi huku wengine
wakijihifadhi kwa Mtendaji wa Kata ya Kirongwe.
Vurugu hizo zinadaiwa kuibuka baada ya wanafunzi saba wa kidato cha
tano kusimamishwa masomo kwa utovu wa nidhamu. Mkuu wa Wilaya hiyo,
Shaibu Ndemanga alisema vurugu hizo zimetokea juzi saa 12 jioni shuleni
hapo na kulazimu askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kutuliza
vurugu hizo zilizodumu hadi saa 8 usiku ambako baadhi ya wanafunzi
walikimbilia kuomba hifadhi kwa mtendaji kata.
“Baada ya hao wanafunzi saba kusimamishwa masomo walitakiwa kwenda
kuwaleta wazazi wao, lakini walikaidi agizo hilo na kubaki shuleni huku
wakiwashawishi wenzao kufanya vurugu kama ishara ya kuwaunga mkono,”
alieleza mkuu wa wilaya.
Alisema Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya inafanya tathmini kujua
uwapo kuna uharibifu wa mali sanjari na kutafuta chanzo halisi cha
vurugu hizo huku Idara ya Elimu Wilaya hiyo ikizungumza na baadhi ya
wanafunzi.
CHANZO : HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment