Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MFUKO wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) wilayani Mwanga, Kilimanjaro,
umeziokoa zaidi ya kaya 350 za vijiji vya Gongoni-Toloha na Karamba Ndea
kwa baa la njaa baada ya miradi yao kuziwezesha kaya hizo kufanya
miradi midogo ya kiuchumi na kujinunulia chakula.
Kadhalika kaya hizo zimefanikiwa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii
(CHF) jambo ambalo awali lilisababisha kutokuwa na uhakika wa kupata
matibabu.
Ofisa Ushauri na Ufutiliaji wa Tasaf wilayani Mwanga, Frednand
Mazuni, alisema kijiji cha Karamba Ndea chenye takribani kaya 520, kaya
200 kati yake zilikuwa na tatizo kubwa la njaa huku baadhi zikila mlo
mmoja kwa siku.
Akizungumzia awamu ya tatu ya Tasaf, wakazi wa kijiji hicho, Palesio
Makange alisema asilimia kubwa ya wananchi wanajishughulisha na biashara
za aina tofauti ikiwamo sukari na nyanya kutoka Mwanga mjini na
kusambaza kijijini hapo na vya jirani.
Awali “Tunaishukuru Tasaf kwani awali wanawake walinyanyasika sana na
mfumo dume, sasa wananunua mazao ya chakula kutoka soko moja kwenda
jingine, faida inanunua vyakula nyumbani,” alisema.
wali wanawake hawakuwa na sauti katika fedha zilizokuwa zikipatikana
kutokana na mifugo kama ng’ombe na mbuzi na kwamba wanaume walikuwa
wakitumia fedha za maziwa na hata kuuza mifugo bila kumshirikisha
mwanamke,” alisema Makange.
Kwa upande wao, wananchi wa vijiji vya Karamba Ndea, Simu Kizungo na
Gogoni Toloha waliomba Tasaf kuwasaidia mradi wa kilimo cha umwagiliaji
ili kuondokana na tatizo la njaa linalowakabili.
Baadhi ya wakazi wa vijiji hivyo, Rukaya Ramadhani na Amina Ali
walisema hali ya kilimo cha kutegemea mvua hakiaminiki na badala yake
wanapata hasara ya mazao yao. Walisema awali mradi huo ulifanyiwa
tathmini kwamba ungegharimu Sh milioni 68 lakini haukutekelezeka
kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao.
CHANZO ; HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment