Anitha Jonas –
MAELEZO
Kilimanjaro
Serikali ya agiza
uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro kujenga
kituo cha kuhifadhi Utamaduni wa wakazi wa Mkoa.
Kauli hiyo imetolewa
leo Mjini Moshi,Mkoani Kilimajaro na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na
Michezo Mhe.Annastazia Wambura alipokuwa
katika ziara ya kikazi mkoani hapo kufuatilia uendeshaji wa shughuli za kisekta
pamoja na kujadili namna ya kuboresha sekta za Wizara .
Mheshimiwa Naibu
Waziri Wambura aliendelea kusema
kuna kila sababu ya kila kwa kila
Mkoa nchini kuwa na kituo cha kiutamaduni ambacho kitahifadhi utamaduni wa
wakazi wake pamoja na kuweka historia ya
maeneo mbalimbali ya kiutamaduni.
“Uwepo wa kituo hicho
utachangia kuongeza utalii wa kiutamaduni pamoja na kukuza pato la mkoa pale
wageni watakapo kuwa wakitembelea vivutio hivyo”,alisema Naibu Waziri
Mhe.Annastazia Wambura.
Pamoja na hayo Naibu
Waziri huyo alitoa maelekezo kwa uongozi
wa mkoa ya kuwataka kuanzisha Kamati
za Maadili katika ngazi ya
Halmashauri na Wilaya zitakazo kuwa zikikagua kazi za filamu za wasanii wa mkoa
kwa kuhakikisha maadili yamezingatiwa na kamati hizo zitafanya kazi kwa
ushirikiano na Bodi ya Filamu Taifa.
Kwa upande wa Mkuu wa
Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick alipokuwa akiwasilisha taarifa ya
maendeleo ya kisekta kwa Mhe.Naibu Waziri alisema Mkoa unakabiliwa na
changamoto ya upungufu wa Maafisa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo lakini
tayari suala hilo wameanza kulifanyia kazi kwa lengo la kuongeza tija katika
sekta hizo.
“Mkoa huu una vivutio
vingi vya kiutamaduni ikiwemo maeneo ya matambiko,eneo alipouwawa mangi Sina wa
Kibosho hivyo uhifadhi wa Utamaduni wa maeneo ni suala zuri na jambo hili
limekuwa likifanywa na nchi zilizoendelea na umewasaidia kuwa ongezea kipato
hivyo suala hili tumelipokea na tutalifanyia kazi”,alisema Bw. Sadick.
Halikadhalika naye
Afisa Elimu Mkoa alieleza kuwepo kwa changamoto ya usikivu wa matangazo wa
Redio kwa Wilaya ya Same na Wilaya ya Rombo.
Pamoja na hayo Mheshimiwa
Naibu waziri alitoa wito kwa watanzania wote kutunza mazingira kwa kuacha
kukata miti hovyo pia kuendelea kuhifadhi maeneo yale ya asili ikiwemo maeneo yanayotumika kwa ajili ya matambiko.
0 comments:
Post a Comment