Naibu Waziri wa
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiwa katika
picha ya pamoja na viongozi na watangazaji wa Kituo cha Redio cha New Life
kilichopo Wilaya ya Hai leo alipowatembelea kuona uendeshashi wa redio hiyo (watatu kulia) ni Askofu Dkt.Eliudi Issangya
na (watano kushoto) ni Meneja Msaidizi wa Redio hiyo Bi. Leah Jackson.
Anitha Jonas –
MAELEZO- Kilimanjaro
Kilimanjaro.
Waandishi wa Habari
watakiwa kutokubali kutumika na wanasiasa
kwa maslai yao binafsi.
Kauli hiyo imetolewa
leo Mjini Moshi,Mkoani Kilimanjaro na Mhe.Naibu Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo alipotembelea Klabu ya Waandishi wa Habari
katika mkoa huo.
“Waandishi nyinyi
ndiyo wenye dhamana kubwa ya kulinda amani ya nchi kwa kupitia taarifa
wanazozitoa katika vyombo vya habari”,alisema Mheshimiwa Naibu Waziri Wambura.
Kwa upande wa Katibu
Mtendaji Klabu ya Wandishi wa Habari Mkoani hapo Bw.Nakajumo James alimuomba
Mheshimiwa Naibu waziri kusaidia klabu hiyo kupatiwa hati ya kiwanja chao
kilichopo Wilaya ya Hai.
“Kupatikana kwa hati
hiyo kutasaidia kukuza kipato cha wanachama kwani tunaweza kupata mikopo
itakayosaidia kuongeza miradi ya klabu”,alisema Bw.James.
Aidha,Katibu huyo
alitoa ombi kwa Mhe.Naibu Waziri la kuomba atoe wito kwa Watendaji na Wasemaji
wa taasisi za serikali kupunguza urasimu katika kutoa habari kwa waandishi
kwani waandishi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto hiyo.
Halikadhalika ziara
hiyo ya kisekta ya Naibu Waziri ilihitimishwa kwa kutembelea Kituo cha Redio cha New Life FM kilichopo
Wilaya ya Hai mkoani hapo kwa leo la kujionea uendeshaji wa sekta ya habari
pamoja na usikivu wa matangazo yake.
0 comments:
Post a Comment