NA. Immaculate Makilika- MAELEZO
Kwa
mujibu wa mtandao wa wikipedia diplomasia ni taratibu zinazoratibu
mahusiano katika ngazi ya kimataifa kati ya nchi na nchi au nafasi za
kisheria nyingine zenye hadhi ya kimataifa, aidha mtandao huu unaendelea
kusema kuwa diplomasia ianaratibu majadiliano baina ya nchi moja na
nyingine hasa pale nchi mbili au zaidi zikipigana, diplomasia husaidia
kusimamisha vita, sambamba na mazunghumzo yanayohusu masuala ya haki, na
amani.
Miaka
ya hivi karibuni diplomasia inatumika pia kwa masuala ya biashara,
uchumi na utamaduni pale nchi zinazoposaini mikataba fulani ya
ushirikiano katika masuala mbalimbali, ambayo huitwa diplomasi ya
uchumi.
Katika
kipindi cha mwaka mmoja cha utawala wa Rais wa Awamu ya Tano,
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli tumeshuhudia ugeni wa viongozi
kutoka mataifa mbalimbali duniani, ni dhahiri kuwa hayo yote yanafanyika
ili kuhakikisha diplomasia inatumika katika kuleta ama kuharakisha
maendeleo hapa nchini.
Oktoba
23 hadi 30 mwaka huu Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco alifanya ziara
ya kikazi ya siku nne nchini, kwa lengo la kukuza uhusiano wa
kidiplomasia kati ya Morocco na Tanzania , ambapo ilisainiwa mikataba
21 ya ushirikiano baina ya nchi hizo, inayolenga kuboresha sekta za
uchumi na teknolojia.
Mikataba
hiyo ni pamoja na makubaliano ya jumla katika ushirikiano wa uchumi,
sayansi, ufundi, na utamaduni iliyosainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Waziri
wa Mambo ya Nje wa Morocco, Mheshimiwa Salahddine Mezouar
Mwingine
ni ule wa kuanzishwa kwa Jukwaa la Mashauriano ya kisiasa baina ya
Wizara ya Mambo ya Nje yaTanzania na Morocco, mkataba wa ushirikiano
katika sekta ya gesi, nishati, madini, uvuvi,sayansi ya miamba pamoja na
ushirikiano katika usafiri wa anga na kuwasaidia wakulima wadogo nchini
kwa kuendeleza soko la mbolea na kilimo kupitia Shirika la Mbolea la
Morocco(OCP) na Shirika la Mbolea la Tanzania.
Kama
hiyo haitoshi, ziara hiyo pia ilitia saini mikataba ya makubaliano ya
mashirika ya Bima ya Tanzania na Morocco, pamoja na ushirikiano
baina ya Bodi ya Utalii Tanzania, Kamisheni ya Utalii Zanzibar na Ofisi
ya Utalii ya Taifa nchini Morocco, ambapo Tanzania inatarajiwa
kunufaika zaidi kwa kupata utaalamu hasa katika sekta ya utalii kwa vile
nchi ya Morocco imekua ikijipatia pato kwa kiasi kikubwa kutokana na
sekta hii.
“Morocco
imepiga hatua kubwa kwenye utalii na kwamba mwaka 2015 ilipokea watalii
milioni 10.5 na mwakani wanategemea kupokea watalii zaidi ya milioni 14
na kwamba Tanzania imeshasaini makubaliano kwenye sekta hiyo kwa
lengo la kuendeleza hifadhi za nchi na kuutangaza utalii” anasema Rais
Magufuli
Sambamba
na hili, mikataba mingine ni kuhusu maeneo maalumu ya uwekezaji (EPZA),
uendelezaji na utangazaji wa viwanda, usafirishaji kwenye reli kupitia
kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (RAHCO) kwa ajili ya ubia
kuendeleza reli ya Mtwara – Mchuchuma/ Liganga, ambapo nchi hizo mbili
kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwenda Rabat, mji mkuu
wa nchi hiyo iliyopo kaskazini mwa Afrika.
0 comments:
Post a Comment