Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani
akiwasili katika eneo lilipo jengo la ghorofa ambalo ni makazi ya sakari
lililoungua moto huku akiongozana na Mwenyeji wake Kamanda wa Polisi
mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa.
Jengo
la ghorof mbili ,makazi ya askari Polisi wa vikosi mbalimbali mjii
Moshi liliungua moto sehemu ya juu na kueteketeza vyumba tisa pamoja na
mali za asakri waliokuwa wakiishi katika vyumba hivyo..
Kamishna
Marijani akiangalia athari iliyotokana na moto katika jengo hilo
ulioteketeza vyumba tisa zikiwmo samani za ndani na nguo za familia za
askari hao.
Kamishna
Marijani akizungumza na CPL Erick Mwantingo mmoja wa askari waliopoteza
vitu vyote vya ndani katika tukio hilo la moto.
Kamishna
Marijani akita pole kwa PC Maswi ambaye pia amepoteza vitu vyote vya
ndani zikiwemo nguo katika tukio la moto lililoteketeza sehemu ya juu ya
jengo hilo.
Kamishna Marijani akimfariji CPL,Simba baada ya kutembelea jengo hilo kujionea athari iliyotokana na moto huo.
Kamishna
Marinaji akimpa pole SGT Hashim baada ya kupoteza vitu vyote vya ndani
pamoja na mavazi kufuatia moto ulioteketeza seheumu ya juu ya jengo
hilo.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akimuongoza Kamishna
Marijani kukagua maeneo mengine ya jengo hilo ambalo linakumbwa na
tukio la moto kwa mara ya pili sasa.
Kamishna
wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi ,Nsato Marijani
akisalimiana na baadhi ya viongozi pamoja na wageni waliofika kwa ajili
ya kutoa pole kwa asakri waliounguliwa vitu katika jengo hilo.
Waliovalia
kiraia ni askari Polisi waliofikwa na janga la kuunguliwa moto vitu vya
ndani pamoja na mavazi wakionekana wenye huzuni.
Afisa
Mnadhimu daraja la kwanza wa jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Koka
Moita akizungumza wakati wa ukaribisho wa Kamishna wa Operesheni na
Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani alipotembelea kambi ya polisi
mjini Moshi.
Kamnada
wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandamizi,Wilbroad
Mutafungwa akitoa taarifa juu ya tukio la moto katika jengo la makazi ya
askari Polisi.
Mkuu
wa Shule ya Polisi,Kamandanti Matanga Mbushi akizungumza wakati wa
kuzifariji familia za askari waliopoteza vitu vyao katika tukio la moto.
Kamishna
wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani akitoa
salamu za pole kwa niaba ya Mkuu wa jeshi la Polisni nchini ,IGP Ernest
Mangu kwa askari waliopoteza vitu vyao wakati wa tukio la moto
lililoteketeza vyumba tisa katika makazi ya askari Polisi mjini Moshi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.
JESHI
la Polisi nchini limetangaza kuwahamisha askari tisa wa vikosi
mbalimbali vya jeshi hilo waliopoteza mali zao wakati wa tukio la moto
lililoteketeza vyumba tisa vya jengo la ghorofa mbili ambalo ni makazi
ya askari.
Mbali
na hatua hiyo jeshi hilo pia limetoa kiasi cha Sh Milioni tisa kwa
familia za askari hao kwa ajili ya kuanza kununua vitu vidogo yakiwemo
mavazi baada ya kutoambulia chochote wakati wa tukio hilo zikiwemo sare
za jeshi hilo.
Kamishna
wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani ametoa kauli
hiyo jana kwa niaba ya Mkuu wa jeshi la Polisi ,Inspekta
Jenerali,Ernest Mangu wakati akizifariji familia za askari hao pamoja na
kutembelea jengo lililoteketea kujionea athari za moto huo uliotokea
usiku wa kuamkia juzi.
Akiwasilisha
salamu za Pole kwa niaba ya IGP Mangu,Kamishna Marijani alisema jeshi
la Polisi litaendelea kutoa msaada kwa askari hao hadi pale maisha yao
yatakaporejea huku akivishukuru vikosi vya jeshi la zima moto vya uwanja
wa ndege wa KIA,kiwanda cha sukari cha TPC na Halmashauri kwa kazi
waliyofanya.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi mwandamizi wa
Polisi,Wilbroad Mutafungwa amemwelea kamishna Nsato kuwa thamani ya mali
za askari zilizoteketea kwa moto imefikia sh Mil 93.9 huku akiomba
wadau kujitokeza kusaidia familia hizo.
Tukio
la moto katika jengo hilo lililopo jirani na ofisi za kikosi cha
kutuliza ghasia lilitokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa 2:30 usiku
,ukianzia katika chumba kimojawapo cha ghorofa ya pili na kuenea katika
vyumba vingine nane wakati huo umeme ukiwa umekatika.
Kufuatia
moto huo familia tisa za askari hao zenye jumla ya watu 40, ambao 23 ni
watu wazima na 17 ni watoto tayari zimepatiwa malazi ya muda katika
chuo cha Polisi Moshi wakati taratibu nyingine za kuwasaidia
zikiendelea.
Tayari
jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limeunda timu ya wataalamu kutoka
katika jeshi hilo wakisaidiana na wale wa kikosi cha zimamoto pamoja na
shirika la umeme (TANESCO) kufanya uchunguzi wa matukio ya moto katika
jengo hilo.
0 comments:
Post a Comment