Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage (Kulia) akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidi wa Uchaguzi Katika Manispaa ya Moshi 20.11.2017. Kushoto ni Mwanasheria Mwandamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Mtibora Selemani.
Na Clarence Nanyaro – NEC
Mwenyekeiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage amewataka
wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi nchini Kuwashirikisha
Viongozi wa Vyama vya siasa katika maamuzi mbalimbali wanayofanya yenye
maslahi kwa pande zote ili kuendeleza amani na utulivu ulipo nchini.
Akizungumza
na Wasimamizi wa uchaguzi katika Manispaa ya Moshi, Jaji Kaijage
alisema kuwa katika kipindi hiki ambapo vyama vinashiriki katika
kampeni za Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakafanyika Novemba 26,2017 ni
muhimu kwa Wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha kuwa Maadili ya Uchaguzi
wakati wa kampeni yanazingatiwa ili kuepusha uvunjifu wa amani miongoni
mwa wananchi.
Jaji
Kaijage ambaye yuko katika ziara ya kutembelea Mikoa ya
Tanga,Kilimanjaro na Arusha kushuhudia utekelezaji wa maadili ya
Uchaguzi katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Udiwani, amewataka
Wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha kuwa Vifaa vyote ambavyo vinahitajika
ili uchaguzi uweze kufanyika vimepatikana na vile ambavyo havijapatika
wawasiliane na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kasoro zinazobainika ziweze
kupatiwa ufumbuzi mapema kabla ya siku ya Uchaguzi.
Wakati
katika mkoa wa Tanga Uchaguzi utafanyika Katika Kata ya Majengo iliyoko
katika Halmshauri ya Mji Korogwe,Mkoani Kilimanjaro,Uchaguzi mdogo wa
Udiwani utafanyika katika Kata ya Bomambuzi katika Manispaa ya Moshi na
Katika Kata za Machame Magharibi ,WeruWeru na Mnadani katika
Halmashauri ya Hai.
Aidha,Jaji
Kaijage alitoa wito kwa Wasimamizi wa Uchaguzi kuhakikisha Kuwa siku ya
Upigaji Kura ulinzi unaimarishwa katika Vituo vya Kupigia kura lakini
usiwe ulinzi wa kuwatia wananchi hofu wakashindwa kufika katika vituo
vya kupigia kura viongozi wanaowataka ili washirikiane nao katika
kujiletea Maendeleo.
0 comments:
Post a Comment