Waombolezaji
wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu, Lulu Sylvester Mattunda
Lema mara baada ya kuwasili nyumbani kwao katika Kitongoji cha
Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi,Wilaya ya Hai,
Mkoa wa Kilimanjaro Januari 25, 2018. Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo
Ijumaa Januari 26, 2018.
Marehemu Lulu Sylvester Mattunda Lema.
Familia katika picha ya pamoja eneo la Korogwe Bararara ya Tanga
Waombolezaji wakiwa nyumbani hapo
Sylvester
Mattunda Lema (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na watoto wake
mara baada ya kuwasili Nyumbani kwao katika Kitongoji cha Nkwelengya,
Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi, Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya
ya Hai kwa taratibu za mazishi yatakayofanyika Leo Saa Nane Mchana,
Januari 26, 2018 katika makaburi ya familia yaliyopo eneo hilo
Mwinjilisti
wa Usharika wa Nronga, Donald Lema akizungumza jambo baada ya mwili wa
marehemu, Lulu Sylvester Mattunda Lema ulipowasili katika Kitongoji cha
Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi, Wilaya ya Hai,
Mkoa wa Kilimanjaro Januari 25, 2018 kwa taratibu za mazishi
yanayofanyika leo Ijumaa Januari 26, 2018 saa Nane Mchana, katika
makaburi ya familia yaliyopo eneo hilo, ambapo Lema alisema, "Katika
mtihani huu ndugu yangu Sylvester,umeshinda katika ile ahadi uliyotamka
ni kifo ndicho kitakacho tutenganisha mimi na wewe Lulu,hivyo ahadi hiyo
umeitimiza, Profesa Lema pamoja na ndugu zako wote nachukua nafasi ya
kuwapeni pole sana na Mungu akawatie nguvu, huyo aliyekufa maisha yake
yamekwisha aliyebaki ndiye ameumia zaidi,wapo ndugu zetu waliokuwa Dar
es Salaam ambao katika msiba huu walishughulika kufa kupona wahakikishe
jambo hili limewezekana kama hivi lilivyowezekana, wapendwa niseme
nivile tunauona msiba tukiusikia kwa mwingine, tumeona mwili umetufikia
nyumbani,kutokana na msiba huu kuna watu wanashughulika
kwa kujitolea kwa hali na mali, wapo wanaotoa matangazo wapo wanaofanya
hili na lile kuhakikisha jambo linakwenda vizuri na wapo waliojitoa kwa
hali na mali ,na kwa wale waliotoka Dar es Sallam na kwa wale waliotoka
ndani na nje ya nchi naomba
kuwashukuru
sana kwaniaba ya ushirika wa Nronga kwa kufanya juhudi zote kuuleta
mwili wa mpendwa hapa nyumba pia napenda kuwaambia mumtie moyo ndugu
yenu pamoja na watoto na mumtegemee Mungu Kwa mioyo yenu yote, huu mwaka
ni mwaka wa marejesho, atarejesha amani
pasipo
amani, atarejesha baraka pasipo baraka, atarejesha afya mahali afya
imetoweka na huu mwaka nimzuri sana kwa anaemtegemea Mungu.
0 comments:
Post a Comment