Home » » 29 WANUSURIKA KUFA KATIKA AJALI K’NJARO

29 WANUSURIKA KUFA KATIKA AJALI K’NJARO



Mwandishi wetu, Kilimanjaro yetu

WATU 29 wamenusurika kufa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka mkoani Arusha kuelekea Tanga kuacha njia na kupinduka katika eneo la kijiji cha Kirinjiko wilayani Same mkoani Kilimanjaro.

Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Robart Boaz amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema imetokea jana majira ya saa 8:00 mchana.

Akielezea ajali hiyo kamanda alisema gari aina ya mistubishi fuso lenye namba T 563 AAQ mali ya kampuni ya Fasaha likiendeshwa na dereva ambae hajajulikana jina likitokea Arusha kuelekea Tanga ikiongozana na basi lenye namba T869 BBA mali ya kampuni ya Hajees liliacha njia na kupinduka na kusababisha ajali hiyo.

Kamanda alisema miongoni mwa majeruhi hao wapo wanaume 16, watoto watano na wanawake wanane  na kuwa majeruhi wanapatiwa huduma katika hospitali ya wilaya ya Same.

Chanzo cha ajali hakijafahamika na kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi na kuwa taarifa za awali zinaonyesha kuwa kuwa gari hilo lilikuwa likikimbizana na gari jingine na kuwa dereva amekimbia mara baada ya ajali hiyo.
Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa