Mwandishi wetu, Moshi
Wakuu wa wilaya na wakurugenzi watendaji wa halmashauri za Wilaya Mkoani Kilimanjaro wameagizwa kuandaa mpango mkakati kwa miezi miwili ijayo ya kuwajengea uwezo wa kuishi watoto wa miataani na wanaoishi katika mazingira hatarishi kama moja ya mkakati ya kuwajengea maisha bora ya baadaye.
Mkuu wa Mkoa Leonidas Gama ametoa agizo hilo katika sherehe za idd el fitiri baada ya kushiriki chakula cha mchana na watoto waishio katika mazingira hatarishi wanaolelewa na kituo cha mkombozi kilichopo mjini moshi
Gama amesema kulingana na utafiti uliofanywa mkoani humo umebaini kuwa zaidi ya watoto hamsini elfu wanaishi mitaani kwa kurandaranda katika wilaya zote za mkoa huo.
Gama amesema kulingana na utafiti uliofanywa mkoani humo umebaini kuwa zaidi ya watoto hamsini elfu wanaishi mitaani kwa kurandaranda katika wilaya zote za mkoa huo.
Aidha amesema kata za karoleni, Njoro, Pasua na Majengo ni miongoni mwa kata za manispaa ya Moshi zinazoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Kutoka na hali hiyo hiyo bwana Gama amesema serikali lazima ichukue hatua za haraka kuwasaidia watoto hao ambapo lengo likiwa ni kuwasaidi wasijiingize kwenye vitendo viovu ukiwemo ujambazi pamoja na utumiaji wa madawa ya kulevya.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment