Home » » AFARIKI DUNIA BAADA YA KUJINYONGA KWA WAYA

AFARIKI DUNIA BAADA YA KUJINYONGA KWA WAYANa Safina Sarwatt, Moshi

MTU mmoja mkazi wa Chekereni, Wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro, Isaack Poul (26) amekutwa amefariki dunia kwa kujinyonga kando kando ya Mto Karanga.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Robert Boaz, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 11 alfajiri, ambapo marehemu alijinyonga kwa kutumia waya.

Kamanda Boaz alisema marehemu hajaacha ujumbe wowote na jeshi bado linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo.

Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mkoa, Mawenzi.

Katika tukio jingine, Jeshi la Polisi linawashikilia watu wa wili, Mwaka Seif (26) na Hadija Seif (30), wote wakazi wa Mbuyuni, Manispaa ya Moshi, kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya kete 30.

Kamanda huyo alisema kuwa watuhumiwa walikamatwa na jeshi hilo juzi katika maeneo ya Mbuyuni na jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi ili kuwafikisha mahakamani.

Chanzo: Mtanzania

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa