Home » » KILIMANJARO YAPAMBANA NA MIHADARATI KWA VITENDO

KILIMANJARO YAPAMBANA NA MIHADARATI KWA VITENDO

Na: Epifania Temu – RS Kilimanjaro

Mkoa wa Kilimanjaro  umeonesha nia na juhudi za kupambana na tatizo la uingizaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya kwa kuwa na kuwakamata wahusika wa uhalifu huo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Akitoa hotuba  wakati wa mapokezi ya mwenge wa uhuru Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Leonidas Gama amesema jumla ya  watuhumiwa   1243  wa dawa za kulevya wamekamatwa katika matukio 831 yaliyohusishwa kukamatwa kwa aina mbalimbali za dawa za kulevya kati ya 2011/2012.

Aidha Mheshimiwa Gama amefafanua kuwa katika kipindi hicho jumla ya kilogramu 224.3 za mirungi kg 14244.7 cocaine kg 7, na  Heroine gramu 239 na watuhumiwa kufikishwa katika vyombo mbalimbali vya sheria.

Mheshimiwa Gama ametaja kuwepo kwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA na mpaka wa nchi jirani ya Kenya, Mkoa wake umejikuta ukiingia katika changamoto za kupambana na tatizo hilo la dawa za kulevya.

Katika kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake Gama, amesema tayari  jumla ya kesi 760 zimefungiliwa mahakamani, kesi182 zikiwa  zimeshughulikiwa na kutolewa hukumu huku kesi 572  zikiwa katika katua mbalimbali mahakamani.

Mwenge wa uhuru umeingia Mkoani Kilimanjaro tarehe 31/07/2012 ukitokea Mkoa wa Manyara ambapo unatarajiwa  kukimbizwa katika halmashauri zote saba zilizomo katika Mkoa huo.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo mwenge wa uhuru, umeanza kukimbizwa  Wilaya ya Same na baadaye  kukabidhiwa Wilayani Mwanga  ambapo utapokewa na Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijjiini.

Utakapomaliza kukimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijini Mwenge wa Uhuru utaelekea Wilayani Rombo ambapo watakabidhi kwa uongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Moshi.

Aidha Halmashauri ya Manispaa hiyo itakabidhi kwa uongozi wa Halmashauri  ya Wilaya ya Hai ambapo wataukabidhi katika Wilaya ya Siha kabla ya kuukabidhi mwenge huo kwa uongozi wa Mkoa wa jirani wa Arusha.

Ukiwa Mkoani Kilimanjaro mwenge wa uhuru unatarajia kufungua, kuzindua, kuweka mawe ya msingi na kutembelea miradi mbalimabli  ya maendeleo ipatayo51 yenye jumla ya zaidi ya Tsh bilioni 4  ambayo imetokana na vyanzo mbalimbali vya fedha .

Akielezea mchanganuo wa gharama za miradi hiyo Mheshimiwa Gama amesema Serikali kuu imechangia Shilingi 2,032,599,724/=, Halmashauri za Wilaya 455,295,775/=, Michango na Nguvu za wananchi 705,062,381/= huku wahisani na wafadhili wakichangia shilingi 892,470,710/=.

Habari na picha kwa hisani ya mdau wetu Shaaban Ally, kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Moshi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa