Home » » POLISI MOSHI WAKAMATA MAJAMBAZI WANNE

POLISI MOSHI WAKAMATA MAJAMBAZI WANNE

Enos Masanja, Kilimanjaro

Jeshi polisi Mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kujihusisha na matukio kadhaa ya ujambazi na mauaji.

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boazi amewataja wanaoshikiliwa kwa tuhuma hizo kuwa ni Said Husein 20, Azizi msangi 44, Peter Brumo 30 na Aloyce Noah 37 wote wakazi wa mjini Moshi.

Kulingana na polisi watu hao walikamatwa wakiwa kwenye harakati za kwenda kufanya uhalifu katika kijiji cha msitu wa tembo wilayani moshi.

Polisi waliandaa mtego wa kuwanasa wahalifu hao mara baada ya kuarifiwa na wananchi na ndipo mtego huo ulipofanikisha kuwanasa watu wane huku wengine kadhaa wakifanikiwa kutoroka.

Pamoja nao jeshi la polisi limekamata bunduki aina ya shortgun iliyokuwa na risasi tano.

Aidha watuhumiwa hao pia wanadaiwa kuhusika na tukio la kifo cha mfanyabiashara mmoja katika kijiji cha mabogini Seleman Hasana aliyeuwawa kwa kupigwa risasi akiwa kwenye duka lake la vileo.

Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi wa tukio hilo kabla ya kuwafikisha mahakamani.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa