Home » » POLISI K’NJARO WAKAMATA MAJANGILI

POLISI K’NJARO WAKAMATA MAJANGILI

Mwandishi wetu, Kilimanjaro Yetu
JESHI la polisi Mkoani Kilimanjaro kwa kushirikiana na askari wa hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro (KINAPA) wamefanikiwa kuwakamata watu wawili wanaotuhumiwa kuwa ni majangili wakiwa na bunduki moja aina ya Refe ikiwa na risasi 10.

Kamanda wa polisi Mkoani Kilimanjaro Robart Boaz amethibitisha kukamatwa kwa majangili hao na kusema wamekamatwa juzi majira ya saa 1:30 asubuhi katika kijiji cha Lerang’wa mpakani mwa wilaya ya Siha
na longido mkoani Arusha.

Kamanda amewataja waliokamatwa kuwa ni Mkonde Mhozya (50) na Ezekel Songoyo (28) wote wakazi wa mkoani Arusha ambapo alisema uchunguzi unaonyesha kuwa majangili hao walikua na lengo la kufanya ujangili
katika mbuga iliyoko katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa kamanda mtuhumiwa Ezekel Songoyo alikuwa akitafutwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa  kosa la kufanya unyanganyi  na kumpora mama mmoja fedha akishirikiana na polisi  katika eneo la benki ya NBC Moshi  mwaka 2010 na kutorokea kusiko julikana.

Akizungumzia tukio hilo Mhifadhi mkuu wa Kinapa Erastus Lufungulo alisema hali ya ujangili wa mazao ya misitu na wanyama bado upo licha ya jithada zinazofanywa na shirika la hifadhi za taifa (TANAPA)
kuhakikisha wanatokomeza ujangili huo.

Lufungulo alisema kwa sasawanashirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha wanalinda misitu na mbuga zote  ili kuzuia vitendo vya ujangili n akusema kwa mwaka jana walifanikiwa kuwakamata majangili 422 na bunduki mbili na mazao ya misitu zikiwemo mbao

Alisema eneo walikokamatwa majangili hao ni eneo linalounganisha mbuga ya Embuseri iliyopo Kenya mbuga ya Kinapa iliyoko Kilimanjaro na mbuga
ya Hifadhi ya Arusha iliyoko mkoani Arusha na kuwa majangili hao walikusudia kufanya ujangili wa wanyama ndani ya mbuga hiyo.

Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa