Home » » TANZANITEONE WAJICHANGISHA KUWASAIDIA YATIMA

TANZANITEONE WAJICHANGISHA KUWASAIDIA YATIMA


na Rodrick Mushi, Moshi
WAFANYAKAZI wa Kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzaniteone kupitia mfuko wao wa Tanzanite Foundation, wamepanda Mlima Kilimanjaro, kwa ajili ya kukusanya fedha za kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Mererani wilayani Simanjaro.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Memeja Mkuu wa kampuni hiyo, Wessel Marais, alisema kuwa safari hiyo itachukua takriban siku tano, ambapo zaidi ya sh milioni 48 zitapatikana.
Alisema kuwa safari hiyo ya kupanda Mlima Kilimanjaro iliambatana na sherehe za miaka 45 tangu kugundulika na kuanza kuchimbwa kwa madini ya tanzanite.
Kampeni ya kuchangisha fedha hizo iliendeshwa na Tanzanite Foundation, ambapo zitaelekezwa moja kwa moja kuwasaidia watoto yatima, wanaosihi katika mazingira magumu na wale wanaoishi na virusi vya ukimwi.
“Tumeamua kufanya harambee hii kwa kupanda Mlima Kilimanajro, ili kupata fedha za kuwasaidia watoto yatima, kitu ambacho kitakuwa kumbukumbu nzuri tangu kugunduliwa kwa madini ya tanzanite,” alisema Marais.
Naye kiongozi wa harambee hiyo, Hayley Henning, alisema kuwa endapo wakiweza kufainikiwa kwenye safari hiyo ya kupanda mlima wanatarajia kuendelea kusaidia zaidi makundi maalumu ya kijamii.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa