Home » » WAHITIMU VYUO VIKUU WATAKIWA KUJIAJIRI

WAHITIMU VYUO VIKUU WATAKIWA KUJIAJIRI



MOSHI
Vijana wanaomaliza elimu ya juu kutoka vyuo mbali mbali hapa nchini wametakiwa kuacha kutagemea ajira kutoka serikalini na mashirika mbali mbali bali watafute mbinu za kuwafanya waweze kujiariri wenyewe

Hayo ni miongoni mwa mapendekezo yalitotolewa na washiriki wa mkutano wa baraza kuu la  24 la YMCA Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa YMCA Moshi mwishoni mwa wiki.

Katika mkutano huo ambao unaongozwa na ujumbe usemao "vijana badilikeni ulimwengu unaongozwa kwa utaalan na kazi wamesema inashangaza kuona baaadhi ya vijana wanamaliza elimu ya juu kutoka vyuo mbali mbali hapa nchini lakini  wanapopewa ajira hawawezi kuifanya kwa ufasana sawa na eluimu waliyoipata.

Wamesema jambo hilo linashangaza sana kwani wao kama wasomi wanategemewa  sana katika kutekeleza mambo mbali mbali hapa nchini hivyo wana wajimbu wa kuhakikisha kuwa wanapohitimi masomo yao katika kani mbali mbali wawe na ujuzi wa kazi hiyo. 

Wakizungumzia utandawazi wamesema, matumizi mabaya ya utandawazi ni miongoni mwa sababu kubwa zinazoleta madhara kwa vijana kutokana na wengi mujiingiza kwenye vitendo viovu na kuharibu maisha yao.

Wamesema utandawazi ni mzuri kama utatumikwa kuwa kujifunza mambo mazuri ikiw ani pamoja na maendeleo badala na kuacha kujifunz mambo mabaya ambayo yanahatarisha uumbaji wa Mungu.

Akionge ana washirki wa mkutano huo Katibu wa YMCA bw Sretewart Lyatuu amesema ni jukumu la wana YMCA kuhakikis akuwa wanahimizana katika kutenda mamambo mema ya kumopendeza Mungu.

Blogzamikoa 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa