Home » » ASASI ZATAKIWA KUTENGA FEDHA KUHIFADHI MAZINGIRA MT. KILIMANJARO

ASASI ZATAKIWA KUTENGA FEDHA KUHIFADHI MAZINGIRA MT. KILIMANJARO

Mwandishi wetu, Kilimanjaro Yetu
Asasi za fedha Mkoani Kilimanjaro zimetakiwa kutenga fungu maalumu kwa ajili ya kusaidia harakati za kuhifadhi mazingira katika maeneo jirani na mlima Kilimanjaro.
Wito huo umetolewa na mdau mashuhuri wa mazingira mkoani Kilimanjaro Bi.Frediel kwayu wakati akizungumza kwenye mahojiano maalum na Radio free Africa ofisini kwake.
Bi. Kwayu amezingatia hali ya kuyeyuka kwa  theluji katika mlima Kilimanjaro na kueleza kuwa hali hiyo itaendelea kuwa  hatarishi kwa  viumbe  hai endapo wadau wote hawata onyesha nguvu kukabili uharibifu  wa mazingira.
Kutokana na hali hiyo Bi.kwayu ambaye anamiliki duka la kubadili fedha za kigeni ameitaka serikali kuhamasisha taasisi zote  za fedha mashika ya serikali na yasiyo ya kiserikali kuanzisha bustani rafiki za mazingira.
Aidha ameshauri miti inayooteshwa igawe bure na kupandwa katika shule za msingi na sekondari lakini pia kwa wadau wengine wanaojihusisha na mazingira.
Mkoa wa Kilimanjaro ni miongoni mwa maeneo yalioathiriwa na uharibifu wa mazingira na duru za kitafiti zinasema mlima huo mrefu kuliko yote barani Afrika utakuwa umepoteza theluji yake ifikapo mwaka 2025 endapo  juhudi madhubuti za kuhifadhi mazingira hazitachukuliwa. 
Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa