Home » » WATU WANNE WAJERUHIWA MAPIGANO YA WANAVIJIJI

WATU WANNE WAJERUHIWA MAPIGANO YA WANAVIJIJI

Na Omary Mlekwa, Siha
WATU wanne wamejeruhiwa kwa silaha za jadi katika mapigano ya kugombea mipaka baina ya wananchi wa vijiji viwili mpakani mwa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro na Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha

Katika mapigano hayo yaliyotokea katika eneo la bonde la Lekrimu lilipo mpakani mwa Kijiji cha Lekrimu wilayani Siha na Rock Ngarenanyuki wilayani Arumeru ambako wakulima wanne walishambuliwa na kujeruhiwa na watu wanaodaiwa kuwa ni wafugaji.

Wafugaji hao wanapinga kuendelea kulimwa eneo hilo kutokana na mgogoro katika bonde hilo.

Kamanda wa Polisi mkoani wa Kilimanjaro, Robath Boaz alisema eneo hilo ambalo lipo mpaka wa vijiji vya Lekrimuni Wilayani na kijiji Rock Ngarenanyuki wilayani Arumeru limekuwa katika mgogoro tangu mwaka 2011.

Baadhi ya wanavijiji walisema mgogoro wa wakulima na wafugaji hao umekuwapo muda mrefu lakini serikali imeshindwa kuutatua hali ambayo wanaamini sasa unaelekea kubaya

Kamanda Boaz alisema tukio lilitokea juzi asubuhi katika maeneo la wazi la bonde la Lekrimu.

Alisema wafugaji na wakulima walianza kupigana kwa kutumia silaha za jadi kupinga wakulima kutoka kijiji cha Rock kuingia katika eneo hilo na kulima licha ya eneo hilo kuzuiwa kufanyiwa kazi zozote hadi utakapomalizika mgogoro huo.

Boaz alisema ugomvu huo ulisababishwa na mmoja wa wakulima wa Kijiji cha Roki kuanza kulima kwa maksai wakati eneo hilo.

Alisema alipotakiwa kuondoka alikaidi na kuendelea kulima jambo ambalo lilisababisha wafugaji kutoka katika Kijiji cha Lekrimu kumtoa kwa nguvu ndipo wakulima wa Kijiji cha Rock walipoingilia na mapigano yakazuka.
Chanzo: Mtanzania

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa