na Dixon Busagaga, Moshi
CHAMA cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Manispaa ya Moshi kimemtaka Mkuu wa
Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, kutumia vyombo vya ulinzi na usalama
kuwakamata na kuwashitaki madiwani kwa kile anachodai ufisadi uliotaka kufanywa
na madiwani hao katika safari yao ya mafunzo Kigali nchini Rwanda.
CHADEMA kupitia
makada wake maarufu, James ole Millya na Jafary Michael walitoa kauli hiyo kwa
nyakati tofauti wakati wa mikutano ya hadhara iliyoanza hivi karibuni katika
maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi kutoa ufafanuzi kwa wananchi wa hatua ya mkuu
huyo wa mkoa kuzuia safari hiyo huku wakiita ni ya kisiasa zaidi.
Mapema mwezi
huu, Gama aliwaambia waandishi wa habari mbele ya kamati ya ulinzi ya mkoa kuwa
amesitisha safari hiyo ambayo ingegharimu sh milioni 123.2.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Penford vilivyoko
katikati ya mji wa Moshi, Meya wa manispaa hiyo, Jafary Ally, alisema fisadi
yeyote anapothibitika anachukuliwa hatua za kisheria.
“Ndugu zangu
wananchi wa Moshi, kama kweli Gama anaona kile madiwani wa CHADEMA walichotaka
kukifanya ni ufisadi….. leo hii hakuna hata mmoja wetu ambaye angekuwa katika
eneo hili la mkutano, wote tungekuwa gerezani.
Alisema mkuu
huyo wa mkoa sasa ameacha majukumu yake ya kiserikali na kuanza kutumika
kisiasa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa lengo la kuwagombanisha madiwani hao
ambao wengi wao wanatoka CHADEMA.
Meya Michael
alisema fedha zilizotengwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo madiwani zitatumika
kama zilivyopangwa na kama mkuu huyo wa mkoa akiendelea kutumika kisiasa na
kuacha shughuli za utendaji wa kuwatumikia wananchi, watatangaza mgogoro naye
wa kutoshirikiana kwenye shughuli zozote.
Chanzo: Taaanzania Daima
0 comments:
Post a Comment