na Dixon Busagaga, Moshi
MENEJIMENTI ya
kiwanda cha sukari cha TPC cha wilayani Moshi, imesema hosptali ya kiwanda
hicho imeanza kutoa huduma za matibabu ya gharama nafuu kwa wakazi wa vijiji
vya jirani vinavyokizunguka.
Ofisa Mtendaji
Utawala, Jafary Ally, alisema hayo hivi karibuni wakati wa ziara ya wanahabari
kutoka klabu ya waandishi ya Mkoa wa Kagera (KPC) waliotembelea kiwanda hicho
kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa.
Alisema mbali
na huduma hiyo ambayo kwa sasa wakazi wa zaidi ya vijiji vinne wananufaika
nayo, pia hospitali hiyo imeendelea kutoa huduma bure kwa wafanyakazi wa
kiwanda hicho pamoja na wategemezi wao baada ya kuboresha eneo hilo.
“Baada ya
kufanya maboresho katika eneo la afya hapa kiwandani, hivi sasa mfanyakazi
anatibiwa bure yeye na watoto wake wanne,” alisema Ally.
Chanzo: Tanania Daima
0 comments:
Post a Comment