Home » » UJENZI WA BARABARA ZA KISASA WAANZA SIHA

UJENZI WA BARABARA ZA KISASA WAANZA SIHA

Mwandishi wetu, Kilimanjaro yetu 
Halmashauri ya wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro imeanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa barabara za majaribio utakaoainisha aina ya teknolojia itakayodumu kwa muda mrefu zaidi.
Miongoni mwa tekonolojia zinazotumika katika ujenzi huo wa barabara ni zile zinazotumia Lami, changarawe na udongo.
Tayari ujenzi wa barabara mojawapo ya Lawate –kibongoto umeanza chini ya ushirikaino baina ya Halmashauri na shirika la maendeleo la uingereza DFID ukigharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.8
Naibu waziri wa TAMISEMI na mbunge wa jimbo la Siha Aggrey Mwandri aliyezuru barabara hiyo ya Lawate-Kibong’oto  yenye urefu wa kilometa 13 ameeleza kuridhishwa na mradi huo na kusema kuwa barabara itakuwa kichocheo kikubwa  cha kukuza uchumi kwa wananchi wanaozunguka eneo hilo.
Mhandisi  wa wilaya ya Siha bwana Meleck Slaa amesema barabara hiyo ni miongoni mwa barabara sita zinazojengwa hapa nchini kwa teknolojia mpya ikiwemo barabara ya Bagamoyo ambazo zitarahisisha usafirishaji na hivyo kukuza uchumi kwa wananchi  hasa katika maeneo ya vijijini.
Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa