Home » » LEMA: NITAHAKIKISHA TANZANIA INAKUWA NCHI YA HAKI

LEMA: NITAHAKIKISHA TANZANIA INAKUWA NCHI YA HAKI

Na Upendo Mosha, Moshi
ALIYEKUWA Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema, amesema atahakikisha Tanzania inakuwa nchi yenye haki na kupambana na mafisadi.

Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana, wakati wa mkutano wa hadhara.

Alisema kwa sasa ubunge si suala la maana kwake na yupo tayari kuhakikisha Watanzania wanatendewa haki, ikiwa ni pamoja na kupinga suala la ufisadi uliokithiri.

“Nitasimama kupigania haki hadi tone la mwisho la damu yangu hadi tutakapoukomesha ufisadi kwa baadhi ya viongozi wa Serikali,” alisema Lema.

Aidha, alisema ipo haja ya vyombo vya usalama na mahakama kusimamia haki.

Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya Moshi Mjini, Jafari Michael, aliwataka Watanzania kuwa na moyo wa uvumilivu katika kipindi hichi cha kudai haki zao.

Alisema Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mjini imetenga zaidi ya Sh milioni 200 kwa ajili ya kuwalipia wanafunzi ada kwa shule za sekondari za kata, kutokana na kuwapo kwa idadi kubwa ya wazazi wasio na uwezo.
Chanzo: Mtanzania

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa