Home » » MSAADA WA HALI NA MALI UNAHITAJIKA KWA HAWA WATOTO...!

MSAADA WA HALI NA MALI UNAHITAJIKA KWA HAWA WATOTO...!


Elia na Elisha ni watoto mapacha na wana umri wa mika 12 na wanasoma darasa la 3 shule ya Msingi Katanini iliyopo Moshi vijijini karibu na shamba la TPC mkoani Kilimanjaro, Watoto hawa wanaishi na bibi na babu yao mtaa wa Matindigani kata ya Pasua mjini Moshi-Kilimanjaro. Hawa watoto walitelekezwa na wazazi wao wakiwa tangu wadogo sana baada ya kutokea kutokuelewana kwa wazazi wao.

Elia na Elisha wanaishi kwenye mazingira hatarishi sana, (hawapati mlo kamili, hawana mavazi, hawana vifaa vya shule) Tangu wameanza darasa la kwanza hawajawahi kulipa ada na wanasoma kwa fadhila za walimu wa shule ya msingi Katanini. Mwaka huu wamepata msaada wa sare za shule ila bado wanamahitaji ya Viatu vya shule, begi la shule, soksi za shule na wanahitaji mtu angalau wa kuwalipia masomo ya ziada kwa kuwa wako nyuma kidogo ya wenzao.
Elia na Elisha hawapati chakula nyumbani kwa sababu bibi na babu hawafanyi kazi na wana mtoto mgonjwa wa muda mrefu hivyo chochote kidogo kinachopatikana hupelekwa kwa huyo mgonjwa.  Kwa kutambua hilo shule ya msingni katanini wamekuwa wakiwapa mlo wa mchana na uji wa saa 4 asubuhi ambapo uji huo ni kwa ajili ya watoto wa darasa la kwanza na pili.

 Natoa wito kwa yeyote mwenye aliyeguswa na matatizo ya watoto hawaanaweza kuwasaidia.  Mahitaji muhimu kama:
·         Chakula.
·         Mavazi.
·         Viatu vya shule.
·         Ada ya  masomo ya ziada. (Tuition)
·         Begi la shule.
·         Soksi za shule.

Unaweza kutoa chochete kati ya vilivyotajwa hapo juu na si lazima utoe fedha. Pia kama una kitu chochote ambacho wewe hauna matumizi nacho mfano nguo ambazo hauzitumii tena badala ya kuzichoma au kuzitupa tafadhali naomba tuzikusanye ili tuwape watu wenye uhitaji. 


Unaweza kupiga namba hizi 0754 090699 au 0712 492131 (John Kessy)
Mwanyekiti wa mtaa 0755 707347 (Renata)

Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wana haki sawa na watoto wengine.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa