Home » » ROMBO WAJENGA KITUO CHA POLISI

ROMBO WAJENGA KITUO CHA POLISI


na Rodrick Mushi, Rombo
WANANCHI wa Kijiji cha Kirongo chini, wilayani Rombo, Kilimanjaro, wameamua kujenga kituo cha polisi kitakachogharimu zaidi ya sh milioni 200 baada ya kukithiri kwa vitendo vya kihalifu na uvunjifu wa amani ikiwemo wizi.
Akizungumza kwenye harambee ya kuchangia kituo hicho, Mwenyekiti wa kijiji hicho, Bartholome Tarimo, alisema ujenzi wake utategemea nguvu za wananchi na wadau wengine pamoja na serikali, ili kusaidia kurudisha amani kwenye kijiji hicho.
Alisema kumekuwepo matukio ya mara kwa mara ya mauaji na wizi ambayo yamejenga hofu kubwa kwa wananchi na kuongeza kuwa Agosti 29, mwaka huu yalitokea mauaji ya kijana, Patrick Kavishe (38) yaliyotekelezwa na watu wasiofahamika.
Kwa upande wake, mgeni rasmi kwenye harambee hiyo, Notburga Maskini, ambaye alikwenda kama mzaliwa wa Rombo, akifanya kazi kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali na Mitaa (Tamisemi), alisema alihamasika kujiunga na wananchi wa eneo hilo kwa uamuzi na ushirikiano waliouonesha kuweza kupata kituo kwenye eneo lao, ili kuwasaidia kuishi kwa amani.
Katika harambee hiyo, zaidi ya sh milioni 6 zilipatikana ambapo ahadi zilikuwa sh milioni 3.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa