Home » » WENYEVITI 260 WA VITONGOJI WAGOMA KUSHINIKIZA POSHO

WENYEVITI 260 WA VITONGOJI WAGOMA KUSHINIKIZA POSHO

Mwandishi wetu, Kilimanjaro Yetu 
Halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro imeingia katika mgogoro na wenyeviti wake  wa serikali za vitongoji ,baada ya wenyeviti hao kususia shughuli zote zitakazopangwa na uongozi wa halmashauri.

Wenyeviti wavitongoji wapatao 260 walikusanyika katika mji wa bomang’ombe na kupaza sauti zao mbele ya waandishi wa habari wakitaka halmashauri yao kulipa mara moja malimbikizo ya posho zao tangu mwaka 2009 yanayofikia shilingi milioni 280.

Miongoni mwa shughuli watakazosusia kulingana na sheria namba 7  ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 ,ni pamoja na kuhamasisha ulipaji kodi na ushuru mbalimbali na kusimamia utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika sekta ya kilimo ,afya na elimu.

Wenyeviti hao wa vitongoji wengi wao wakitokea chama cha mapinduzi CCM, wamekariri sheria namba 7 ya  serikali za mitaa inayoeleza kanununi zinazoongoza halmashuari ulipaji wa posho na kushangazwa na hatua ya halamashuari yao kuendelea kupuuza matakwa ya kisheria.

Pamoja namgogoro huo,halmashauri ya wilaya ya Hai pia imeingia katika mzozo mwingine na madiwani wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mwishoni mwa wiki iliyopita  walisusia kikao cha baraza la madiwani baada ya mkurugenzi huyo kudaiwa kuitisha kikao bila makubaliano na mwenyekiti wake.

Mkurugenzi wa Halamashuari ya wilaya ya Hai bwana bw. Melkizedek Humbe alipofuatwa na Radio free Afrika kutoa ufafanuzi wa masuala hayo hakuwa tayari kuyazungumzia akiahidi kutoa maelezo baada ya kukamilika kwa zoezi la sensa ya watu na makazi linalohitimishwa septemba 8 mwaka huu.
 Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa