Home » » WAHAMIAJI HARAMU 10 WAKAMATWA KILIMANJARO

WAHAMIAJI HARAMU 10 WAKAMATWA KILIMANJARO

Na Upendo Mosha, Moshi
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro, linawashikilia wahamiaji haramu 10 kutoka Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria. Mbali na wahamiaji hao, pia linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kuwasafirisha wahamiaji hao katika eneo la Kilemapofo na Mjohoroni, wilayani Moshi.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Koka Moita, alisema Septemba 6, saa tisa usiku katika eneo la Kilemapofo wilayani Moshi, zilikamatwa pikipiki nne zilizowapakia wahamiaji haramu wanane.

Alisema wahamiaji hao ambao wamebuni mbinu nyingine za kutumia usafiri wa pikipiki, walikamatwa wakiwa wametokea eneo la Tarakea wilayani Rombo kueleka wilayani Hai, ambako walikuwa wamepanda pikipiki hizo kwa mtindo wa mshikaki.

Akizungumzia tukio jingine, alisema Septemba 6, mwaka huu, saa tisa katika eneo hilo walikamata pikipiki tatu zikiwa zimewabeba wahamiaji wengine sita wakitokea wilayani Rombo kuelekea wilayani Hai.

Alisema wakati askari wakijaribu kuwatia nguvuni watu hao, wahamiaji haramu wanne walifanikiwa kutoroka na kufanikiwa kuwakamatwa wahamiaji wawili pamoja na madereva wa pikipiki hizo.

Aidha, alisema madereva wa pikipiki hizo wanashikiliwa kwa tuhuma za kuwasafirisha wahamiaji haramu kinyume cha sheria na watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.
Chanzo: Mtanzania

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa