Home » » WALEMAVU WAPANDA MLIMA KILIMANJARO

WALEMAVU WAPANDA MLIMA KILIMANJARO

Walemavu watatu kutoka nchini Ufaransa waliopanda Mlima Kilimanjaro, Roman Soler (kushoto), Laurence Aclocque (wa pili kushoto) na Domminique Verami Colas (wa kwanza kulia), muda mfupi kabla ya kuanza safari yao kuelekea kilele cha Mlima Kilimanjaro

Na Mwandishi wetu

Katika kuudhihirishia ulimwengu kuwa ulemavu si kikwazo kwa binadamu kuishi na kutenda kama walivyo binadamu wasio na ulemavu, raia watatu kutoka nchini Ufaransa, wamepanda Mlima Kilimanjaro.

Raia hao wa kigeni, walifanya hivyo juzi wakiwa na hamu ya kufikisha ndoto yao ya miaka mingi ya kufika kileleni mwa Mlima Kilimanjaro.

Waliopanda kwa kupitia njia maarufu ya Marangu ni Domminique Veranni Colas (51), mlemavu wa miguu; Roman Soler (28), mlemavu asiyeona na Laurence Aclocque (50), mlemavu wa kutosikia.

Wanatarajia kushuka Septemba 16, mwaka huu kwa kutumia njia ya Mweka ambapo safari yao inaratibiwa na Kampuni ya Nature Discovery.
Chanzo: Nipashe

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa