Home » » Wanahabari watembelea taasisi ya utafiti wa zao la Kahawa TACRI mkoani Kilimanjaro

Wanahabari watembelea taasisi ya utafiti wa zao la Kahawa TACRI mkoani Kilimanjaro

 Mtafiti katika taasisi ya utafiti wa zao la Kahawa Tanzania,TaCRI 
kanda ya kaskazini ,John Mabagala akiwaelezea wanahabari kutoka mkoa 

wa Kagera aina mpya za miche ya Kahawa ililiyo fanyiwa utafiti katika 

kituo hicho.

 Meneja wa programu ya uongezaji tija wa ubora wa Kahawa na msimamizi 
wa maabara ya udongo TaCRI,Godsteven Maro akiwalelezea wanahabari  jinsi maabara hiyo inavyo fanya shughuli zake.

 Mtafiti katika taasisi ya utafiti wa zao la Kahawa Tanzania,TaCRI 
kanda ya kaskazini,John Mabagala akizungumza na wanahabari kutoka 

mkoa wa Kagera waliotembelea Taasisi hiyo kujionea jinsi inavyo fanya 

shughuli zake.zira hiyo iliandaliwa na muungano wa vilabu nchini UTPC 
na kuratibiwa na klabu ya wanahabari mkoa wa Kilimanjaro,MECKI.

 Waahabari kutoka Mkoani Kagera wakiendelea kutembelea taasisi ya utafiti wa zao la Kahawa nchini TaCRI kujionea shughuli mbalimbali zinzofanywa na taasisi hiyo.

Na Dixon Busagaga waglobu ya jamii Moshi.


WANAHABARI sita kutoka klabu ya wandishi wa habari mkoa wa 
Kagera(KPC)wametembelea taasisi ya utafiti wa zao la Kahawa nchini 

TaCRI kujionea shughuli mbalimbali zinzofanywa na taasisi hiyo.



Ziara hiyo iliyoandaliwa na muungano wa klabu za waandishi wa habari 
nchini(UTPC) na kuaratibiwa na klabu ya waandishi wa habari mkoa wa 

Kilimanjaro MECKI ilikuwa na lengo la mafunzo kwa wanahabari kujifunza 
na namna gani waandishi wa mikoa mingine wanavyo fanya shughuli zao 
ikiwa ni pamoja na jinsi wanavyoshirikiana na wadau.



Wakiwa katika taasisi hiyo ,wanahabari hao walipata maelezo kutoka kwa 
Mtafitio John Mabagala kuhusiana na shughuli zinazofanywa na kituo 

hicho na baadae walipata fulsa ya kutembelea maeneo mbalimbali kituoni 
hapo ikiwemo Maabara ya Udongo,Vitalu vya miche ya Kahawa na maktaba 
ya taasisi hiyo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa