Na Florah Temba,
Moshi-Kilimanjaro Yetu
ASKARI polisi hapa
nchini wametakiwa kufanyakazi kwa kufuata sheria, maadili
na misingi ya polisi nchini ikiwa ni pamoja na kuepuka matumizi ya nguvu
na silaha za moto katika kutekeleza majukumu yao ili kuepuka matukio ya
kuua raia.
Mkuu wa jeshi la
polisi nchini IGP Saidi Mwema aliyasema hayo wakati akifunga
mafunzo ya uongozi mdogo jeshini katika chuo cha taaluma ya polisi
moshi ambapo alisema suala la ulinzi na usalama katika nchi
ni jukumu la kila mtanzania pasipo kujali nafasi na cheo alicho nacho .
Alisema polisi
wanapaswa kuangalia ulazima na umuhimu wa kutumia nguvu katika utekelezaji wa
majukumu yao ikiwa ni pamoja na kufuata sheria na kwamba polisi atakayekwenda
kinyume atawajibishwa kwa mujibu wa kanuni na sheria za jeshi hilo.
Alisema uwajibikaji
wa polisi na wananchi ni jambo la msingi hususani katika kipindi hichi
ambacho jeshi hilo linaupungufu mkubwa wa askari ambapo askari mmoja analazimika
kuhudumia wananchi 1300 badala ya wananchi 400 kama inavyopaswa kidunia
Aidha alisema takwimu
zinaonyesha kuwa asilimia 89 ya watanzania hawana ufahamu wa kutosha kuhusiana
na suala la ulinzi na usalama na badala yake wanaamini kuwa jukumu la usalama ni
la Polisi na viongozi jambo ambalo si sahihi.
“Ulinzi na usalama ni
jukumu la kila mmoja na si la polisi wala viongozi pekee,watanzania wote
tuwajibike katika kulinda ulinzi na usalama wa nchi,na katika hili tutafanikiwa
kukomesha matukio ya kiuhalifu na kuimarisha amani na utuli” alisema Mwema.
Kwa upande wake kaimu
mkuu wa chuo cha taaluma ya polisi Bw.Robert Boaz alisema jumla ya
askari 2825 kati ya 2865 wamefanya vizuri mitihanai yao na kupandishwa
vyeo wakati 41 wamefeli na kutakiwa kurudia kwa wiki moja na watakao faulu ndio
watapandishwa vyeo
Naye kaimu mkuu
wa mkoa wa kilimanjaro Bw..Elinas Palanjo alisema askari wasijivunie vyeo
walivyovipata bali watambue kuwa vyeo hivyo ni majukumu na
wanapaswa kuyatekeleza kwa mujibu wa sheria na taratibu.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment