Home » » MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AMEWATAKA VIONGOZI WABOVU KUCHUKULIWA HATUA KALI

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AMEWATAKA VIONGOZI WABOVU KUCHUKULIWA HATUA KALI

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama amewataka viongozi katika ngazi mbalimbali serikalini kuwachukulia hatua kali watendaji ambao hawa zingatii maadili na nidhamu kazini. Aliyasema hayo, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa baraza la watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mjini Moshi jana.
Alisema nidhamu kazini, ndiyo msingi wa mafanikio hivyo viongozi wote wanapaswa kuwaajibisha watendaji wabovu.

Alisema viongozi kushindwa kusimamia maadili na nidhamu kazini, ni kushindwa kutimiza wajiu unaostaili kwa mujibu wa sheria na kanuni.

“Napenda kutoa wito kwa viongozi kuchukua hatua kali bila kusita kwa yeyote ambaye hazingatii maadili na nidhamu kazini, hatua hii tasaidia kurudisha uwajibikaji mzuri kwa watendaji na tutailetea nchi yetu maendeleo na kuondokana na umasikini”alisema

Aliwataka watendaji wa ofisi hiyo, kutumia changamoto walizonazo kama frusa ili kufanya kazi kwa bidi na kuhakikisha maatizo hayo yanatatuliwa bila kuitegema serikali.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dk. Albina Chuwa alisema hivi sasa wanakabiliwa na changamoto ya ukosekanaji wa mfumo thabiti wa kuratibu utoaji na usambazaji wa takwimu kitaifa.


CHANZO GAZETI LA MTANZANIA 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa