Home » » Serikali yatakiwa kuimarisha benki

Serikali yatakiwa kuimarisha benki



SERIKALI imeandaa mpango madhubuti wa kuziimarisha na kuziendeleza benki za ushirika nchini, ili kuzijengea uwezo wa kuwahudumia wakulima kwa kuvipa mikopo vyama vikuu vya ushirika, badala ya kuzitegemea taasisi nyingine za fedha. Hayo yalibainishwa na Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Tanzania, Peter Rutabanzibwa wakati wa mkutano mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Kilimanjaro (KNCU).


Alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa benki hizo, zinafikia kiwango cha juu kuwahudumia wakulima na kwamba jukumu la wanachama wa vyama vyote vya ushirika nchini ni kuziunga mkono benki hizo.

Alisema kutokana na benki hizo kutokuwa na uwezo mkubwa wa kukopesha wakulima, wengi wamekuwa wakikimbilia benki zote za ushirika kwa kuwawezesha wakulima kukopa katika benki hizo kwani tumekuwa tukishuhudia wakulima wetu wakinyanyasika katika taasisi nyingine.

Nao baadhi ya wajumbe wa mkutano huo, walieleza kutoridhishwa kwao na mwenendo wa utendaji wa Benki ya Ushirika mkoani hapa, kwa kuwashawishi wakulima kutengana na KNCU na hivyo kuvuruga ushirika.

Walisema baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo, wamekuwa wakifanya semina za kuvishawishi vyama vya msingi vya ushirika vijitenge na KNCU katika biashara ya kahawa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa KNCU, Maynard Swai amewataka wajumbe hao kutoa tamko juu ya benki hiyo na kupendekeza wajumbe wawili wa Bodi ya Wakurugenzi wa KNCU kuingia kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo ili kudhibiti hali hiyo.

Alisema chama hicho, kimeimarisha mtaji wa benki hadi kufikia Sh milioni 153.6



CHANZO: MTANZANIA
.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa