Mbali na magunia hayo jeshi hilo pia linamshikilia mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Jackson Arold (19) kwa tuhuma za kukutwa na misokoto 250 ya Bangi.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz, alisema Magunia hayo yalikamatwa Julai 31 mwaka huu majira ya saa kumi na nusu
alfajiri katika kijiji cha Ngare Nairobi mpakani mwa Kenya na
Tanzania, yakiwa yamepakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T.977 ACB aina ya Land Rover.
Kamanda Boaz alisema magunia hayo ya Bangi yalikamatwa na askari wa usalama barabarani ambapo baada ya kuliona gari na kulishtukia walilisimamisha na baada ya kusimama watuhumiwa waliokuwa na gari hiyo walitoka na kukimbia kusiko julikana na kulitelekeza gari hilo.
Inaelezwa kuwa kuwa Gari hilo lilikuwa likielekea nchi jirani ya Kenya ambako inadaiwa kuna Biashara nzuri ya Madawa hayo ya Kulevya aina ya Bangi.
Akielezea tukio la pili kamanda Boaz alisema misokoto hiyo iliyokuwa kwenye begi la mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina la Jackson Arold (19), ambaye ni mkazi wa Mbokomu ilikamatwa Julai 30 mwaka huu katika eneo la Kiboriloni.
Kamanda Boaz alisema kukamtwa kwa mtuhumiwa huyo lilitokana na taarifa zilizotolewa na Raia wema baada ya kutilia mashaka begi ambalo alikuwa amelibeba mtuhumiwa huyo.
Aidha kamanda aliongeza kuwa jeshi lake limejiimarisha katika ulinzi hasa katika maeneo ya mipaka ili kuweza kuzuia kuingizwa na kutolewa kwa madawa ya kulevya ndani na nje ya Mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni moja ya mikakati ya kutokomeza biashara hiyo katika mkoa huo na taifa kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment