MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji nchini (Ewura),
imepandisha bei ya maji katika mji wa Moshi na viunga vyake huku ikitoa
masharti kwa Mamlaka ya Maji safi na Maji taka mkoani hapa (Muwsa), kuchimba na
kutekeleza miradi mitatu ya uchimbaji wa visima vipya.
Taarifa ya Ewura iliyotolewa na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu, Haruna
Masebu, kwenda Muwsa inaonesha mamlaka hiyo imeridhia ongezeko hilo la bei mpya
ya maji kutumika kuanzia Agosti mosi mwaka huu.
Kwa mujibu wa agizo hilo la Ewura, ongezeko la bei ya maji safi na ma
jitaka kati ya mwaka 2013/2014 linawajumuisha wateja wenye dira katika kundi la
majumbani, taasisi, biashara, viwanda, magati na kuosha magari.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ambayo Tanzania Daima imefanikiwa kuiona,
mamlaka hiyo imepandisha pia bei ya kumwaga maji taka kwa maboza kutoka sh
10,000 hadi sh13,000 kwa mwaka 2013/2014 .
Katika kundi la wateja wa majumbani wenye dira za maji bei imepanda
kutoka sh 412 kwa mita za ujazo hadi kufikia sh 495 kwa mwaka 2013/2014. Wale
wanaoosha magari bei imepanda kutoka sh 597 kwa mita hadi sh 715,” Ilieleza
taarifa hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Muwsa, Mhandisi Cyprian Luhemeja alithibitisha
taarifa za kupanda kwa bei ya maji huku akikiri kuwapo kwa agizo la Ewura la
kurekebisha bei ya huduma ya maji kuanzia Agosti mosi mwaka 2013.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment