KIJIJI cha Chekereni Weruweru Wi l a y a y a Mo s h
i mk o a n i Kilimanjaro, kimetajwa kuongoza kwa wizi wa maji, hali ambayo
imekuwa ikiisababishia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi
(MUWSA) kupata hasara
.Hayo yalibainishwa jana na Ofisa Uhusiano wa MUWSA,
Dorah Kilo wakati wa operesheni ya kuwabaini wananchi wanaojiunganishia maji
kinyume cha sheria na taratibu, jambo ambalo limekuwa likiisababishia mamlaka
kupata hasara kubwa.
Kilo alisema kwa siku Mamlaka hiyo huzalisha mita
za ujazo 1,200 za maji katika kijiji hicho lakini asilimia 80 ya maji hayo
hupotea, kutokana na baadhi ya wananchi kujiunganishia maji kinyume cha Sheria
na taratibu.
"Kumekuwepo na upotevu mkubwa wa maji katika
kijiji hiki, kwani kwa siku tumekuwa tukizalisha maji mita za ujazo 1,200,
lakini asilimia 80 ya maji hayo hupotea, na upotevu huu husababishwa na watu
kujiunganishia maji kinyume cha sheria," alisema.Alifafanua kuwa Mamlaka
hiyo kwa sasa hupoteza asilimia 28 ya maji yanayozalishwa ambapo asilimia 80 ya
upotevu huo inatoka katika kijiji cha Chekereni Weruweru.
Alisema katika operesheni waliyoifanya kwenye
Kijiji hicho changamoto kubwa waliyokutana nayo ni wananchi kujiunganishia maji
kinyume cha sheria, jambo ambalo limekuwa likisababisha kuendelea kuwepo kwa
upotevu mkubwa wa maji.
"Katika operesheni tuliyoifanya, tumekutana na
changamoto kubwa ya mkazi mmoja kujiunganishia maji isivyo halali na amechimba
kisima, lakini pia amepandisha maji kwenye tanki kwa kutumia mota jambo ambalo
ni kinyume cha sheria, kwa kweli hii ni hujuma kubwa kwa Mamlaka na serikali
kwa ujumla," alisema Kilo.Kutokana na hali hiyo mamlaka hiyo ilimtaka
msimamizi wa eneo hilo kuhakikisha kiwango cha upotevu wa maji kinapungua
ifikapo mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.
Aidha Dorah alitumia pia nafasi hiyo kuwaasa wakazi
wa Kijiji cha Chekereni Weruweru, kuacha mara moja tabia ya kujiunganishia maji
kinyume cha sheria na kwamba kwa yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua kali
za kisheria ikiwa ni pamoja na kusitishiwa huduma ya maji.
"Niwatahadharishe wananchi wa eneo hili,
waache haraka sana kujiunganishia maji kinyume cha sheria, kwani hatua ya
kwanza tutakayoichukua kwa mtu atakayebainika kufanya hivyo, ni kumkatia maji
kwa mujibu wa sheria na kumtaka alipe gharama ambazo zilipotea kutokana na wizi
wa maji aliokuwa akiufanya," alisema.
Akizungumza
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Katanini Kijiji cha Chekereni Weruweru, Yahaya
Salum aliwataka wananchi kutoa
ushirikiano kwa mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira MUWSA, na kuhakikisha
wanawafichua wale wote ambao wamekuwa wakijiunganishia maji kinyume cha Sheria
ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Chanzo: Majira
0 comments:
Post a Comment