Asia Ramadhan akiwa na mwanaye Rajabu Hassan (14) ambaye miguu yake
imepinda na kumsumbua hadi kushindwa kujiunga na kidato cha kwanza
mwakani.
Unaweza kufikiri ni hadithi, lakini ukweli ni kwamba watoto
wengi wanaozaliwa kijijini Mtakuja Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro,
wengi wao wamepinda miguu, kuharibika ubongo na wengine kupata meno
yenye rangi ya kahawia.
Tatizo hili limekuwepo kijijini hapo kwa muda mrefu sasa na kukiathiri kijiji hiki kilichopo kilometa 25 kutoka Bomangíombe, Makao Makuu ya Wilaya ya Hai.
Ukubwa wa tatizo
Ni kwa watoto kuzaliwa na vichwa vikubwa, matatizo ya ubongo na wengine ambao miguu yao imepinda.
Sababu kubwa inaelezwa kuwa ni kunywa maji ya visima yenye kiasi kikubwa cha madini aina ya Fluoride.
Mzee Selestine Shayo (67) ambaye ameishi kijiji hapo tangu mwaka 1964, anasema wamekuwa wakinywa maji hayo bila kujali kiwango cha madini hayo.
Anaeleza kuwa maji hayo kimsingi hayafai hata kwa matumizi ya mifugo.
Asia Ramadhan (31) ni mama wa watoto watano, lakini mmoja kati yao, Rajabu Hassan (14) ameathirika, yeye alianza kupinda miguu alipokuwa darasa la tatu mwaka 2009.
ìMwanzo mwanangu alilalamika kuwa mifupa ya miguu inapasuka, ndipo tukampeleka Hospitali ya Mawenzi na baadaye wazungu waliokuja hapa wakatupa dawa, ndipo akapata nafuu kidogo,î anasema.
Anaongeza kuwa baada ya kufanyiwa vipimo na madaktari wakamweleza kuwa mtoto wake amepata matatizo hayo kutokana na maji wanayokunywa kijijini hapo ambayo yana madini mengi aina ya Fluoride.
Mama huyo anamshukuru Mungu kwa kuwa mtoto wake amefaulu mtihani wa darasa la saba mwaka huu katika Shule ya Msingi Mtakuja na kupangiwa Shule ya Sekondari Kia.
ìKutoka hapa hadi Kia ni kilometa sita, ukiongeza zile za kurudi ambazo pia ni sita, mtoto wangu hatoweza kujiunga na masomo ya sekondariÖMifupa ya miguu haitaweza kutembea umbali wote huo,î anasema.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Makao Mapya, Pili Hamisi (56) ni bibi anayemlea mjukuu wake aitwaye Juma Hamza (8) ambaye ni mlemavu wa viungo na ubongo kutokana na matumizi ya maji hayo.
ìBaada ya kuzaliwa, kwa miezi tisa hakukaa wala kuonyesha dalili ya kutambaa, nikampeleka KCMC (Hospitali ya Rufaa), pia Mawenzi ambako madaktari wakaniambia kuwa akifikisha umri wa miaka mitano ataweza kutembea,î anasema.

Anaongeza: “Kweli alipofika umri huo akatembea
japo kwa shida, viungo vimelegea na mpaka sasa hajaweza kuongea na wala
hawezi kula chakula mwenyewe… yote tunamwachia Mungu.”
Mwenyekiti huyo anaeleza kuwa eneo hilo lina
karibu watoto 20 ambao wote wamepinda miguu na madaktari walimweleza
kuwa kiini cha tatizo hilo ni maji wanayokunywa yana kiwango kikubwa cha
Fluoride.
“Wapo waliozaliwa wazima, lakini baada ya miaka
michache wakapata tatizo la kupinda miguu na wengine wanakufa. Hata juzi
juzi tulizika hapa watoto wawili… kweli inauma,” anasema Pili.
Hali katika Shule ya Msingi Mtakuja inashtua kwani watoto wasiopungua 20 wamepinda miguu.
Mwalimu Method Haule anapiga kengele na kuagiza
watoto watoke nje ambako kwa hesabu ya haraka, wasiopungua 20 wana
matege ya waziwazi.
“Hapa nina watoto kama 20 wamepinda miguu, lakini
tatizo ni maji…haya maji ya visima yana Fluoride nyingi sana… naona kuja
kwako (mwandishi) utakuwa ukombozi kwetu,” anasema.
Wenye vichwa vikubwa hufungiwa ndani hadi kufa
Wenyeji wa kijiji hiki ambao ni wafugaji wa
Kimasai na wakulima wa makabila mchanganyiko, wanadokeza kwamba wapo
watoto wenye ulemavu ambao wanafichwa.
“Wenzetu (Wamasai) wakipata mtoto mwenye kichwa
kikubwa ama aliyepinda miguu, wao husema ni mokii (laana) wanawafungia
ndani hawapati huduma mpaka wengine wanakufa,” anaeleza Leslie Makundi.
Mkazi mwingine wa kijiji hicho, Christopher Shao,
maarufu Kimeta, anasema inahitajika kazi ya ziada kutoa elimu kwa
wananchi wa kijiji hicho ili wasiwafungie watoto wao ndani wawapeleke
shule.
“Kumficha mtoto si suluhisho kwa sababu hii sio
laana kama wanavyofikiri… inatakiwa waonekane ili na Serikali nayo ijue
tuna tatizo na inapaswa kuchukua hatua kuokoa wananchi wake,” anasema.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment