Home » » Watatu wafa ajalini Moshi

Watatu wafa ajalini Moshi

Moshi. Watu watatu wamefariki dunia papohapo baada ya kugongwa na basi la Kampuni ya BM Coach, lililokuwa likitokea Morogoro kwenda Arusha eneo la Gezaulole, wilayani Hai.
Waliofariki dunia ni mwendesha pikipiki na watembea kwa miguu, waliokuwa pembezoni mwa barabara ya Moshi-Arusha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alithibitisha kuwapo kwa ajali hiyo na kwamba, chanzo ni mwendesha pikipiki kuingia ghafla barabarani bila kuchukua tahadhari.
“Ni kweli kuna ajali imetokea kwenye saa 11:40 hivi pale Wilaya ya Hai, kuna mwendesha pikipiki aliingia ghafla barabara kuu… dereva wa basi akajitahidi kumkwepa bila mafanikio,” alisema.
Boaz alisema baada ya kumgonga mwendesha pikipiki huyo ambaye alikufa papohapo, basi hilo liliyumba na kwenda kuwagonga watu wengine watano huku wawili wakifariki papohapo.
Kamanda Boaz, alisema watu watatu waliojeruhiwa katika ajali hiyo walipelekwa Hospitali ya Rufani ya KCMC kwa matibabu, hadi tunakwenda mitamboni taarifa ya hali zao ilikuwa haijajulikana.
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa