Home » » MTOTO AFUNGWA KAMBA KUZUIA ASITOROKE

MTOTO AFUNGWA KAMBA KUZUIA ASITOROKE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

MTOTO Samir anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka minne hadi mitano, mkazi wa Mtaa wa Langoni katika Manispaa ya Moshi, amekuwa akifungwa kamba mguuni na bibi yake kwa lengo la kumzuia asiende kucheza mbali.
Tukio hilo limebainika hivi karibuni katika eneo hilo ambapo bibi huyo ambaye hakufahamika jina alikutwa akiwa amemfunga kamba ya mguu mjukuu wake huyo huku sehemu nyingine ikiwa imefungwa katika chuma kizito.
Kwa mujibu wa majirani walisema bibi huyo amekuwa akimfunga mtoto huyo mara kwa mara kwa zaidi ya nusu saa hasa nyakati ambazo bibi huyo amekuwa akifanya shughuli zake za usafi wa ndani pamoja na kufua.
Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina, majirani hao walisema imekuwa ni kawaida kwa bibi huyo ambaye anaishi na wajukuu zake kumfanyia kitendo hicho mtoto huyo huku akimzuia kucheza na wenzake wa nyumba za jirani.
“Sisi hiyo hali mbona tumeizoea mara kwa mara Samir akienda kucheza na wenzake huko mitaani, bibi yake akimkuta anamkamata na kisha kumfunga kwenye hilo chuma lililoko hapo mlangoni kwa zaidi hata ya nusu saa,” alisema mmoja wa majirani.
Akizungumza tukio hilo, bibi huyo ambaye anakadiriwa kuwa na miaka zaidi ya 60 alikiri kumfunga mtoto huyo kwa madai amekuwa mtundu kupita kiasi na kwamba ametumia mbinu hiyo ili kumdhibiti asitoroke nyumbani.
“Hapa nyumbani naishi na wajukuu zangu, wengine wako shuleni na wengine wako kazini ambao ni wazazi wa huyu Samir, mmoja anafanya kazi Arusha, mwingine yuko hapo mjini (Moshi) sasa sina mtu wa kunisaidia kumwangalia huyu mtoto,” alisema bibi huyo.
Alisema analazimika kumfunga kamba mtoto Samir kutokana na kuwa na tabia ya kwenda kuzurura katika nyumba za watu huku wakati mwingine huenda kucheza mbali na nyumbani, jambo ambalo humpa shida kumpata kwa urahisi.
Chanzo;Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa