Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Moshi Vijijini, imekana ahadi yake iliyotoa
mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda mwaka 2009, ya kumlipa mkandarasi
aliyejenga kituo cha polisi kilichopo Kijiji cha Mkomilo Kaya ya Okaoni.
Uchunguzi uliofanywa ma TanzaniaDaima umebaini kuwa kituo hicho
kilijengwa kwa nguvu ya wananchi kwa ushirikiano na jeshi la polisi
nchini na tangu kizinduliwe mwaka 2010, na Rais Jakaya Kikwete,
mkandarasi huyo hajalipwa zaidi ya sh. milioni 90.
Akizungumza na gazeti hili juzi, Mkurugenzi wa Kampuni ya SAMM
Construction, Elikunda Msaki, alikiri kutolipwa fedha alizotumia katika
ujenzi huo na kutishia kwenda mahakamani kuomba ridhaa ya makahakama
imrejeshee majengo hayo.
Juzi mkurugenzi wa halmshauri hiyo, Fullgence Mponji alikana
halmashauri yake kutoa ahadi hiyo huku akidai kuwa mwenye dhamana ya
kumlipa mkandarasi huyo ni yule aliyeingia naye mkataba wa ujenzi ambao
ni wananchi wa tarafa ya Kibosho.
Halmashauri hiyo iliahidi kubeba gharama za ujenzi wa kituo hicho
mbele ya Pinda ambaye aliweka jiwe la msingi la ujenzi wake,
ulioasisiwa na wanachi wa tarafa ya Kibosho waishio jijijini Dar es
Salaam baada ya kukithiri kwa matukio ya ujambazi wa kutumia silaha
ulioambatana na mauaji ya raia.
Wakati mkurugenzi akikana halmashauri yake kutoa ahadi hiyo,
mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Morris Makoi aliwaambia waandishi wa
habari hivi karibuni kuwa halmashauri yake inao wajibu wa kumlipa
mkandarasi huyo na kwamba tayari mwaka jana walimlipa sh. milioni 30 kwa
ajili ya kupunguza deni.
Alisema kuwa halmashauri yake ilipanga kuweka fedha kwa ajili ya
kumlipa mkandarasi huyo kwenye bajeti yake ya mwaka wa fedha 2013/2014
lakini hadi sasa haijafanya hivyo.
Mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa katika mkutano mkuu wa 29 wa ALAT
Taifa uliofanyika Mei mwaka jana jijini Arusha, Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia aliiagiza halmashauri hiyo kuweka
kwenye bajeti yake deni la mkandarasi huyo.
Kituo hicho chenye hadhi ya daraja B, ujenzi wake umegharimu zaidi ya
sh. milioni 300, ambako Jeshi la Polisi nchini lilichangia sh. milioni
70 huku mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa kiuto hicho, Cyril Makoi
akichangia zadi ya sh. milioni 16 na nguvu ya wanachi ikiwa zaidi ya sh.
milioni 100.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment