Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAZIRI
Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya ameushauri uongozi wa Benki ya Wananchi
Mwanga (MCBL) kuibadili kutoka benki ya wananchi na kuwa ya biashara ili
ya kupanua wigo na kufungua matawi kwenye mikoa mingine.
Msuya alitoa ushauri huo hivi karibuni alipokuwa akichangia namna ya
kuifanya MCBL kukua katika mkutano mkuu wa 14 wa mwaka uliofanyika
wilayani Mwanga, Kilimanjaro.
“Ningependa kushauri MCBL ibadilishe utoaji huduma zake kutoka benki
ya wananchi na kuwa benki ya biashara… itasaidia kupanua wigo wake na
kufungua matawi mikoani,” alisema.
MCBL ilitangaza mafaniko yake kibiashara kwa kupata faida ya sh
milioni 68 kwa mwaka wa fedha 2012/2013 licha ya changamoto nyingi
zinazoikabili.
Akizungumza kwa njia ya simu na Tanzania Daima jana Mkurugenzi
Mtendaji wa benki hiyo, Abby Ghuhia, alisema faida ya mwaka 2013
imeshuka ikilinganishwa na mwaka 2012 kutokana na gharama za uendeshaji
kuongezeka baada ya kufungua vituo vya huduma Moshi Mjini na Same.
Aliongeza kuwa mtaji wa hisa umeongezeka kutoka sh milioni 555 hadi sh milioni 567 sawa na ongezeko la sh milioni 12.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment