Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbunge wa Jimbo la Hai,Freeman Mbowe
Ilidaiwa kuwa Mbowe alishindwa kufika hapo kutokana na kuachwa na ndege.
Akizungunza mbele ya hakimu Agnes Muhina mdhamini wa Mbowe, Awazi Urono, alisema mwenyekiti huyo alishindwa kufika baada ya ndege aliyotarajia kusafiria kumuacha.
“Mheshimiwa hakimu, Mbowe ameshindwa kufika mahakamani kwa sababu gari lake limepata hitilafu wakati akielekea uwanja wa ndege (Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere-JNIA)…Aliachwa na ndege iliyokuwa inakuja KIA kwa hiyo naomba ichukuliwe kama udhuru na taarifa rasmi ya mahakama,” alisema Urono.
NIPASHE ilishuhudia mahakamani hapo wananchi wakifurika kwa lengo likiwa kusikiliza kesi ya Mbowe anadaiw akumshambulia Nassir Yamin ambaye alikuwa ni mwangalizi wa ndani katika uchaguzi huo. Baada ya taarifa hiyo, Hakimu Muhina alisema mahakama imepokea rasmi ujumbe huo kama taarifa ya mahakama na kwamba kesi hiyo imeahirishwa mpaka Novemba 8, mwaka huu.
“Kwa kuwa mdhamini wa Mbowe yupo, dhamana ya mshitakiwa inaendelea kama kawaida, lakini pia naamini upande wa utetezi umejipanga vizuri kuhusu mashahidi na vielelezo.,” alisema Hakimu Muhina
Katika kesi hiyo ya jinai namba 73 ya mwaka 2011, Mbowe akiwa mmoja kati ya wagombea ubunge wa jimbo la Hai, anadaiwa kumshambulia Nassir Yamin katika Kijiji cha Nshara, Kata ya Machame Kaskazini, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro
Katika uchaguzi huo, Mbowe aliibuka mshindi kwa kupata kura 28,585 akifuatiwa na Fuya Kimbita (CCM) kura 23,349, Hawa Kihogo (UDP) kura 258 na Petro Kisimbo (TLP) 135.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment