Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
CHAMA Kikuu cha Ushirika mkoani Kilimanjaro (KNCU), kimeishutumu ofisi ya Mrajisi wa vyama vya ushirika nchini kikidai ni kikwazo katika ustawi wa ushirika kutokana na kuyumba katika utoaji wa uamuzi.
Shutuma hizo zilitolewa hivi karibuni na Mwenyekiti KNCU, Maynard Swai katika mkutano mkuu maalumu ulioitishwa na mrajisi, kujadili hoja za ukaguzi ambazo ofisi hiyo imedai chama hicho kimeshindwa kuzijibu kwa muda mrefu.
Swai, alidai kuwa ofisi hiyo ya mrajisi imekuwa ikitoa uamuzi tata ikiwamo kuzuia uuzwaji wa shamba kubwa la kahawa la Gararagua, ambalo KNCU kililenga kuliuza ili kulipa mkopo wa benki ya CRDB na madeni ya vyama vya msingi pamoja na kujiimarisha kifedha.
Alisema pamoja na kumshirikisha mrajisi katika mchakato mzima wa uuzwaji wa shamba hilo na ofisi yake kuridhia kwa barua ya Machi 27 mwaka huu, lakini iligeuka na kusitisha mchakato huo.
Swai, alisema utata wa uamuzi huo ni uvunjifu wa sheria namba 6 ya ushirika ya mwaka 2013, kifungu cha 132 (3) kinachoweka bayana kuwa mtu yeyote anayekwaza au kuingilia shughuli za ushirika na kuisababishia hasara atawajibika kwa hasara hiyo.
Kutokana na mkanganyiko huo, KNCU wanadai kuwa watalazimika kulipa riba na marejesho ya milioni 250 mapema Novemba mwaka huu, baada ya Mei mwakani.
Kuhusu mgogoro wa shamba la Lyamungo, KNCU wanadai kuwa ofisi ya mrajisi imeshindwa kutekeleza maagizo ya aliyekuwa Waziri wa Ushirika, George Kahama, kwamba shamba hilo ni mali yao katika barua yake ya Oktoba 21 mwaka 2005.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment