Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mtalii huyo aliyepooza upande wa kushoto wa mwili wake, alitumia siku sita kufika kituo hicho kupitia njia ya Marangu inayofahamika kama ‘Coca Cola’ kutokana na kuwa na hali za uwanda tofauti kabla ya kufika kwenye kilele cha mlima huo mrefu kuliko yote barani Afrika.
Murakanil, jana alikabidhiwa cheti namba 10,347 makao makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, (Kinapa), muda mfupi baada ya kushuka kutoka mlimani huo wa kipekee ulimwenguni unaosimama wenyewe
bila kuwa na safu za milima (free stand mountain).
Akizungumzia tukio hilo, alisema hakupata shida sana kupanda mlima huo kwani alikuwa akitumia kiti chake, ingawa alikuwa ana mauimivu kwenye maeneo mbalimbali ya mwili hasa kwa kuwa amepooza upande mmoja.
“Kama sehemu ni nzuri nilikuwa natumia baisketi yangu ya magurudumu matatu, lakini kwenye yale maeneo korofi nilikuwa navutwa na muongoza utalii na wapagazi ndiyo maana nina maumivu mwilini,” alisema mtalii huyo.
Murakanil, aliambatana na rafiki yake kupanda mlima huo, Onuori Keniji, ambaye alidai kuwa hii ni mara ya pili Murakanil kupanda mlima huo, kwani mwaka uliopita alijaribu bila mafanikio, kwani aliishia kituo cha Mandara.
Kwa upande wake muongoza utalii kutoka kampuni ya uwakala wa utalii ya JJM, Aron Teete, alisema kuwa alishirikiana na wapagazi 14 kuhakikisha mtalii huyo anafika kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro.
“Mnasikia anasema yeye hajachoka sana ila sisi ndiyo tumechoka sana, kwani tulifanya kazi ya ziada kuhakikisha anafika kileleni kwa kusukuma baiskeli yake na kwenye sehemu mbaya ilipomlazimu kutembea, ilibidi tumvute kwa kamba,” alisema Teete.
Naye Meneja wa JJM, Julius Mlay, alisema wana uzoefu wa kuandaa safari za mlimani kwa watalii wenye ulemavu, kwani mwaka jana walifanikisha kuwapandisha watalii watano wenye ulemavu wa miguu wakitumia baiskeli za magurumu matatu huku watatu wakitumia miguu ya bandia.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment