Home » » EMBUKOI WAPANIA MAPINDUZI SEKTA YA ELIMU

EMBUKOI WAPANIA MAPINDUZI SEKTA YA ELIMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MWENYEKITI wa Kijiji cha Embukoi wilayani Siha Mkoa wa Kilimanjaro, Lazaro Lengere, amesema kwamba wamejipanga kuleta mapinduzi kwenye sekta ya elimu kwa kujali usawa wa kijinsia, kitu ambacho miaka ya nyuma ilikuwa tofauti.
Kijiji hicho, asilimia kubwa ya wananchi wake ni jamii ya wafugaji, ambako Lengere alisema kuwa wamepiga hatua katika sekta ya elimu, ikiwemo kujitolea katika michango ya maendeleo na kuwapatia watoto elimu bila kuchagua jinsia.
Lengere, akizungumza katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima, alisema kwa sasa wapo katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo, ikiwemo agizo la Rais la ujenzi wa  maabara katika shule ya Sekondari ya Sikirari iliyopo kijiji hapo.
Mwenyekiti huyo ambaye ameongoza Kijiji hicho kwa zaidi ya miaka 30, alisema kwa sasa tayari wamekwishakubaliana kwenye mkutano wa Kijiji, kila kaya kuchanga sh 10,000 kwa ajili ya ujenzi wa maabara.
Hata hivyo, katika hatua nyingine Langere alisema kuwa Kijiji kimetenga eneo la ekari 22, kwa ajili ya ujenzi wa shule, zahanati, ofisi ya kijiji, kanisa pamoja na shughuli nyingine za maendeleo kwa miaka ijayo.
Alisema kumekuwepo na upotoshwaji ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya wananchi wasiopenda maendeleo kuwa, eneo hilo lililotengwa kwa shughuli za maendeleo limeuzwa, kitu ambacho hakina ukweli wowote, bali wanafanya hivyo kwa lengo la kumchafua.
Kwa upande wake, Mtendaji wa Kata ya Orkolili, Maiko Molel, alisema kuwa wananchi kwenye Kata hiyo wanapata huduma ya maji safi na salama kwenye vijiji vyote vya Embukoi, Donyomurwa, Orkolili na Ormelili, nishati ya umeme.


Molel, alisema kwa upande wa afya, wananchi wamekuwa wakitumia zahanati ya Manyatapamoja na hospitali ya Wilaya, huku wananchi wa Kijiji cha Embukoi wakiwa wameshapeleka maombi Halmashauri ya ujenzi wa zahanati, pamoja na kutenga eneo.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa