ONGEZEKO la watu kuzunguka Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro
(Kinapa), limeathiri mazingira na kutishia kutoweka kwa msitu wa nusu
maili.
Hayo yamo kwenye taarifa ya Mhifadhi wa Kinapa, Erastus Lufungulo
alipozungumza na waandishi wa habari waliotembelea miradi ya kijamii
inayofadhiliwa na hifadhi hiyo chini ya Idara ya ujirani mwema katika
sekta ya elimu, afya, maji na mazingira.
Alisema kukithiri kwa uharibifu wa mazingira katika ukanda wa nusu
maili kumeathiri mfumo wa ikolojia na maji ambako baadhi ya uharibifu
huo ni kusogezwa kwa eneo la ukanda huo.
Kwa mujibu wa Lufungulo, eneo la nusu maili limepungua kutokana
kilometa za mraba 88.18 tangu ilipoanzishwa mwaka 1941 hadi kilometa za
mraba 51.2 kulingana na mabadiliko ya mipaka yaliyofanyika mwaka 2005.
Athari nyingine ni ongezeko la matukio ya moto katika msitu wa asili
kwa upande wa juu yaliyosababisha eneo hilo kuwa vichaka vifupi na
kupungua kwa uoto wa asili.
Mhifadhi huyo alisema juhudi zinafanywa kwa ushirikiano na Mkuu wa
Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama aliyepiga marufuku watu kukata miti
kwa ajili ya mbao bila kibali kutoka ofisini kwake.
Chanzo:Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment