SERIKALI Mkoa wa Kilimanjaro ipo mbio kuhakikisha kaya zote za
wakazi wa mkoa huo zinajiunga na Bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa
(iCHF) ili kupata matibabu muda wote.
Akizungumza hivi karibuni katika hafla ya uzinduzi wa mfuko wa iCHF
mkoani hapa jana, alisema mpango wa serikali ni kuhakikisha kila kaya
nchini Tanzania inakua mwanachama wa mfuko huo.
Katika hotuba ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Mtumwa
Mwako ilisema serikali iko katika hatua za mwisho kuupeleka muswada huo
bungeni ambao utalazimisha kila kaya ijiunge na bima ya afya.
“Muswada umeshapitishwa na Baraza la Mawaziri na sasa umepelekwa
kwenye kamati ya Bunge ya huduma za jamii kabla ya kusomwa rasmi
bungeni,” alisema na kuongeza maboresho ya CHF yamekuja muda muafaka.
Akizungumza katika hafla hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mkurugenzi wa iCHF, Athuman Rehani alisema
Mfuko huo umekasimiwa na serikali mamlaka ya kusimamia mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa.
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mkurugenzi wa iCHF, Athuman Rehani alisema
Mfuko huo umekasimiwa na serikali mamlaka ya kusimamia mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa.
Alisema NHIF imelenga ifikapo mwaka 2015
asilimia 30 ya watanzania wote wawe wamejiunga na mfuko huo huku akibainisha kwamba hadi Septemba mwaka huu, asilimia 16.5 ya watanzania wanatumia bima hiyo.
asilimia 30 ya watanzania wote wawe wamejiunga na mfuko huo huku akibainisha kwamba hadi Septemba mwaka huu, asilimia 16.5 ya watanzania wanatumia bima hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Siha, Rashid Kitambulilo
alisema mpango huo umefanikiwa kwa sababu tayari familia 431 zimejiunga
na iCHF.
Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment