SERIKALI imeunda Tume ya Maridhiano itakayoshughulikia chanzo cha
mgogoro baina ya mwekezaji wa Ndarakwai na wafugaji wa kimasai walivamia
na kuchoma moto nyumba 16 katika shamba la mwekezaji huyo mwezi
uliopita.
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu alipokutana na kamati
za ulinzi na usalama za mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, alisema namna
pekee ya kupata ufumbuzi wa tatizo hilo ni mazungumzo kupitia tume
ambayo itaishauri serikali ili ichukue hatua zaidi.
“Naomba tusitoe mwanya kwa tatizo hili kuendelea, lengo la serikali
ni kuhakikisha inalipatia ufumbuzi haraka ili kila mmoja aishi kwa amani
bila machafuko,” alisema waziri huyo.
Alisema serikali itaendelea kuthamini michango ya wawekezaji wa ndani
na nje waliopo nchini huku akitoa maazimio kwa tume hiyo yatakayoleta
suluhisho kwa pande.
Miongoni mwa maazimio hayo ni kujua watu walioshiriki kusababisha
athari za uharibifu wa mali za mwekezaji huyo na uhalali wa eneo hilo na
kuondoa migogoro inazojitokeza hifadhini.
kuondoa migogoro inazojitokeza hifadhini.
Novemba 14 mwaka huu, shamba la kampuni ya Tanganyika Film and
Safari, mali ya Peter Jones lilivamiwa ambapo magari tisa na nyumba 16
vyenye thamani ya sh bilioni 1.7 viliichomwa moto na wafugaji wa kimasai
wakigombania malisho ya mifugo
Chanzo:Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment