kazini
Mafundi wakiendelea na na kazi ya ujenzi wa Mradi wa gati mpya ya Kiwira katika Ziwa Nyasa, Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya juzi.
Wachuuzi na wafanyabiashara wa mazao ya chakula katika soko la
Gonja-Maore, lililopo Kata ya Maore wilayani Same, Mkoa wa Kilimanjaro,
wamelitelekeza soko la kisasa lililojengwa kwa Sh80 milioni kwa kile
kilichodaiwa kukosekana kwa miundombinu muhimu.
Soko hilo lililojengwa na Serikali kupitia mradi
wa Tasaf awamu ya pili, lilizinduliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge
Novemba 2014, Rachel Kasanda lakini mpaka sasa wafanyabiashara wa maeneo
hayo wamegoma kulitumia soko hilo kwa kukosekana kwa huduma ya maji.
Wakizungumza juzi baadhi ya wafanyabiashara,
Fatuma Hussein na Mwajuma Ally walidai kuwa wafanyabiashara wamegomea
soko hilo kwa sababu limejengwa mbali na makazi ya wananchi na hivyo
wananchi wengi huishia kununua bidhaa zinazouzwa mtaani na kwa
wanaotembeza.
Walidai mbali na sababu ya umbali pamoja na
ukosefu wa maji, pia soko hilo halijajengewa uzio jambo linalowafanya
wafanyabiashara hao kuhofia mali zao kuibwa.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Maore, Mbura
Omar, mbali ya kukiri kuwapo kwa kasoro zilizopo, alisema uongozi mpya
wa kijiji hicho umejipanga kuingilia kati sakata hilo ili kuhakikisha
changamoto hizo zinatatuliwa na wafanyabiashara wanauza biashara zao
ndani ya soko.
Diwani wa kata ya Maore, Hamad Sempombe alisema
kuwa hakuna mfanyabiashara au mchuuzi atakayeruhusiwa kuendesha biashara
nje yasoko hilo, na kwamba kwa sasa wamepanga kukutana na
wafanyabiasharaili kuona ni jinsi gani ya kutatua changamoto hizo na
kujenga umojautakaowafanya wafanyabiashara kutii sheria za kuuza bidhaa
sokoni nasio barabarani
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment