Home » » Upinzani waibana serikali kufungua shule za sekondari.

Upinzani waibana serikali kufungua shule za sekondari.


Waziri Kivuli wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Susan Lyimo.
Waziri Kivuli wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Susan Lyimo (Chadema), (pichani), amesema kufungwa kwa shule za sekondari za bweni za serikali kutokana na ukosefu wa chakula na kwamba viongozi husika wa serikali wanapaswa kuwajibiswa badala ya wakuu wa shule hizo.
 
Kutokana na hali hiyo, ameitaka serikali kuharakisha kuzifungua shule hizo ili kuwanusuru wanafunzi wa kidato cha sita walioko nyumbani na wanatarajia kuanza mitihani yao ya Taifa mwezi ujao.
 
Kauli hiyo inakuja siku chache, baada ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sigini, kuwaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri, Manispaa na Majiji kuwachukulia hatua walimu wa shule kuwa hawakustahili kutangaza kufungwa kwa shule, bali kuwasiliana na wakurugenzi ambao ndiyo wenye mamlaka.
 
Alisema walimu wakuu wa shule hizo hawapaswi kuwajibishwa kwa sababu hawana fungu lolote la fedha, kwa kuwa zinatoka katika halmashauri, hivyo walimu wakuu ni watekelezaji tu.
 
“Sioni sabau ya kuwaadhibu walimu wakuu kwa sababu wao hawatoi fedha, serikali ndiyo inayopaswa kubeba lawana katika suala hili,” alisema Lyimo.
 
Aliongeza kuwa Serikali inapaswa kuboresha miundombinu ya barabara na reli ili kurahisisha usafirishaji wa vyakula kutoka katika mikoa yenye chakula cha kutosha na kupeleka katika maeneo yenye uhaba wa chakula ikiwamo mashuleni.
 
Aidha, Lyimo ameitaka serikali pia kutoa maelezo ya kina kuhusiana na kuchelewa kutangazwa kwa ajira za walimu, ambapo kwa mujibu wa Lyimo ajira hizo zilipashwa kutolewa Februari mwaka huu.
 
CHANZO: NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa