Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, kimetoa
siku saba kwa wapangaji waliopo kwenye vibanda vya maeneo ya chama
hicho, kulipa kodi la sivyo, hatua kali zitachukuliwa kwa watakaokaidi
agizo hilo.
Akizungumza na gazeti hili jana mara baada ya kumalizika kwa kikao
cha Kamati ya Siasa, Katibu wa Itikadi na Uenezi wilaya ya Hai, Fadhili
Juma, alisema kikao hicho kimefikia muafaka huo kutokana na kuwapo
usumbufu wa ulipaji kodi kwa wafanyabiashara hao.
Alisema wafanyabiashara hao ni wale waliopo eneo la Uwanja wa
Sabasaba ambao idadi yao ni 148, na eneo la ofisi za chama hicho wapatao
48, na kubainisha waliolipa kodi ni wafanyabiashara sita tu.
Juma alisema baada ya Kamati ya Siasa kukaa vikao vingi kwa muda
mrefu bila mafanikio kwenye suala la ulipaji na kutii masharti ya
mikataba iliyopo, hivyo kikao kimetoa agizo kwa wafanyabiashara hao wawe
wamelipa kodi wanayotakiwa kulipa kulingana na makubaliano ndani ya
siku saba.
Alisema baada ya muda uliotolewa kupita, chama kitatumia watu wenye
mamlaka ya kukusanya kodi hizo ili kufanikisha mpango huo na makusudio
ya wafanyabiashara wote kulipa kodi.
Alisema kwa sasa ni muda mrefu maeneo ya CCM yametumiwa na watu
kufanya biashara zao, lakini chama kimekuwa hakinufaiki kwa chochote
hali inayosababisha kushindwa kujiendesha katika ngazi ya wilaya.
Juma aliwataka wafanyabiashara hao kutambua muda wa kubembelezana
umekwisha, na maeneo ya chama hicho hayawezi kugeuzwa shamba la bibi
ambalo kila mmoja anafanya biashara zake na kujipatia kipato lakini
hataki kulipa kodi kwa mhusika.
CHANZO ; HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment